1)Kujiamini: hii tabia humfanya ajithamini siku zote na kuitambua thamani yake. Kamwe hatojihisi dhaifu au kujiona cheap.
Wanawake wasiojiamini siku zote ni dhaifu mno na huwa hujiona hawana thamani hivyo huwa cheap na wengi huishia kuharibiwa maisha.
2. Ujasiriamali: hii ni tabia ya mwanamke ambayo humtofautisha yeye na jini chuma ulete, akiwa na tabia hii huwa na mikakati ya kusaka hela na kupiga kazi kuongeza kipato hivyo hatarajii kamwe kuwa tegemezi au mzigo kwa mmewe.
3. Uaminifu: hii ni tabia ambayo humfanya kuwa mtiifu kwa mmewe na ndoa yake hivyo kuwa mama kamili na mke mwema kwa mmewe. Mwanamke asiyejitambua huwa na usaliti mwishowe huleta matatizo katika familia yakiwemo magonjwa kama UKIMWI.
4. Nidhamu ya matumizi: hii ni tabia wanayomis mabinti wengi wa kisasa ambao wao suala la kuzingatia matumizi limekua gumu, wao hujali outing, disco, night club, simu za gharama, mitindo ghali na maisha ya kifahari kuliko hata uwezo na vipato vya waume zao hivyo wengi huishia kuchepuka. Tabia ya nidhamu ya matumizi huepusha hasara. Mwanamke mwenye tabia ya nidhamu ya matumizi ni mwanamke anaefaa sana kwa maendeleo ya familia.
5. Kuridhika: hatamani cha mtu, huridhika na kile Mungu alichomjalia mmewe na familia yake. Hii husaidia kujenga familia yenye furaha na amani pasipo usaliti.
6. Usafi: tunaposema mwanamke mazingira tunamaanisha ajitambue na kuhakikisha usafi wa hali ya juu wa tabia, mwili, mavazi, chumbani, mmewe, watoto na nyumba huyo ndio mwanamke wa grade A.
7. Ukarimu: kwa wageni, ndugu, wazazi, wakwe na marafiki wa familia. Hapo ndipo tunapopata tafsiri kamili kuwa mwanamke ni MALAIKA tukiwa na maana kuwa uwepo wake ndani ya nyumba hufunika familia kwa vazi la upendo, ukarimu na faraja. Amani na furaha hutawala familia yenye mwanamke wa aina hii.
8. Usikivu: kwa mmewe na wazazi na hata majirani pale anaposhauriwa mambo yenye tija kwa familia yake.Humsikiliza mmewe na kujadili nae mambo mema na mipango yao ya familia pamoja huku wakipeana mawazo na ushauri. Wanawake wengi miaka hii wamejaa viburi, jeuri na ubishi kiasi kwamba hujiona wao ndio kila kitu ndani ya nyumba hawaambiliki wala hawashikiki.
Ntaendelea kuzitaja sifa za mwanamke BORA siku nyingine ila kwa leo naomba niishie hapa, kama umenielewa SHARE post hii na marafiki zako wapate funzo hili.
Nakutakia siku Njema Mungu Akubariki na kukulinda
Usisahau ku LIKE na kui SAVE page hii ili usipitwe na habari mpya za kila siku, kwa maoni, ushauri au jambo lolote usisite