Nmepita maeneo mengi nmekuta familia nyingi zikisambaratika kutokana na wanaume kutotambua nafasi yao katika nyumba, wengi wamepotoshwa na utandawazi na sera za wanaharakati wa haki za binadamu wanaozunguka kila mahali wakisema haki sawa hivyo majukumu na maamuzi ya kifamilia yanayotakiwa kuamuliwa na wanaume sasa wake zao ndio wanaamua. Wanaume wameishia kunywa pombe na kuchepuka nje huku wakilalamika kuwa ndoa ni mateso tupu miaka hii.
Wanawake nao hususani walioajiriwa na walio wasomi wengi wamevimba vichwa na kuwa kama TEMBO katika familia zao yaani hawaambiliki wala hawashauriki, wanabishana na waume zao mbele ya watoto, ndugu na majirani na wengine hufikia hata kupigana na waume zao, HII NI LAANA hakika Mungu hapendi maana hata vitabu vitakatifu vinasema MUME NI KICHWA CHA FAMILIA hata uumbaji alitangulia kuumbwa Adam ndipo akafuata Eva sasa iweje leo wanawake mnasahau nafasi zenu katika familia na kujivika vilemba vya udikteta na ufalme??!!!!!......
Nafasi ya mwanamke kwa mmewe yapaswa kujikita katika mambo yafuatayo:
1) kumshauri
2)kumfariji, kumheshimu, kuwaheshimu ndugu zake, wazazi wake yaan wakwe zako, kumjali, kumthamini na kuyaheshimu mawazo yake pasipo kuyakosoa kwa shari na matusi bali upole, hekima na utii.
3)kumlea kimapenzi, usafi, kumsifia, sala na maombi.
4) kumzalia watoto na kumtunzia familia, hapa wengi wamejisahau siku hizi wamewaachia ma housegirl majukumu yote wao wapo bize na whatsapp, Facebook na instagram.
5)kumtuliza kimawazo, kiakili, kumpikia, kumlisha, kumvisha, kumuogesha na hata kuhakikisha unakua nae popote inapobidi kimapumzko OUT kutoa stress, hapa siku hizi wanawake wengi wamewaachia mabaamed, masecretary na mahousegirl
Yapo mengi ila hayo ni baadhi ya mambo muhimu mke apaswayo kuyazingatia kwa mmewe.
#Mwanaume
Pia mwanaume tambua kuwa, "Familia ikiyumba wewe mume ndio wa kulaumiwa, ndoa ikisumbua wewe mume ndio wa kulaumiwa, hakuna mwingine ni wewe mwanaume". "Ndoa ama familia yako vikiyumba wewe ndio sababu kutokana na mambo mawili: moja inawezekana ulishindwa kuchagua mke mwema: pili inawezekana umeshindwa kumsimamia mke wako ili awe mwema. Yote mawili(kushindwa kuchagua na kushindwa kusimamia) ni makosa yako na huna wa kumlaumu". Niwashauri vijana wa kiume ambao bado hamjaoa, "Msikosee kuchagua" pili ninawashauri wanaume mliokwisha oa, "Wasimamieni kwa bidii na uaminifu wake zenu , "Wema ama ukorofi wa mwanamke alieolewa umo katika matendo na tabia za mumewe"
Bila shaka naamini nimeeleweka.
Imepenya.. Haijapenyaaaaa?????....
Kama imepenya jibu #IMEPENYAAAA kisha LIKE page hii twende sawa.
Nakutakia siku Njema Mungu Akubariki na kukulinda