-->

Hiki Ndicho Kinachoitwa Kichaa Cha Mapenzi


Vijana wengi huamini kwamba, baada ya kukutana kimwili, ndipo wanaweza kudai kwamba, hao ni wapenzi wao na kwamba kukutana kimwili, ndiyo mapenzi au kupenda kwenyewe.

Inapotokea wanapokutana huvutiwa na tendo la ndoa, huamini kabisa kwamba, uhusiano nao utakuwa mzuri. Kwao, tendo la ndoa ndio kipimo cha uimara wa uhusiano wao.

Baada ya kufanya mapenzi, wapenzi hao huamini kwamba, sasa wanaweza kujitolea kwenye uhusiano huo na kwamba, wanaweza kuwa na nguvu nao kwa asilimia kubwa.

Suala hili, kuna wataalamu huliita mtego wa kimapenzi. Huitwa hivyo, kwa sababu huwafanya wapenzi kutokuangalia sifa nyingine na badala yake kuweka nguvu kwenye mwili, yaani tendo la ndoa.

Upofu hutokea kutokana na kuzalishwa kwa kemikali nyigi mwilini, zenye kumfanya mtu asiweze kujiuliza kuhusu maeneo mengine ya kimasha ya binadamu, zaidi ya mwili.

Kinachotokea ni mwili kuvutwa na wale tunaowapenda kwa kuzalisha homoni inayofahamika kama ‘phenylethylamine’ au PEA kwa kifupi.

Kemikali au homoni hii pamoja na nyingine kama vile ‘depomine’ na ‘norepinephrine’ (ambazo huchochea hali za kimwili) na ‘ testosterone’(ambayo huongeza hamu ya kujaamiana), huzalishwa mara baada ya kukutana kimwili.

Baada ya kuzaliswa kwa homoni hizi, akili ya mtu huona mwili tu, yaani mapenzi na siyo sifa nyingine. Hapa ndipo ambapo, mtu hujikuta hawezi kujizuia tena kukutana kimwili na mpenzi wake, mara baada ya kukutana naye mara ya moja.

Baada ya kufanya mapenzi na kufikia kileleni, huzalishwa homoni iitwayo ‘oxytocin’ (ambayo huhusika na mihemiko), homoni hii humfanya mtu kujikuta anapenda kuwa karibu na kujifungamanisha na mtu aliyefanya naye mapenzi. Tunaweza kusema, ukaribu kwa wapenzi wawili huongezeka na unakuwa ni ukaribu wa mwili zaidi.

Kuzalishwa kwa homoni hizi, ni jambo ambalo mtu hawezi kulizuia na huwa linakuja kwa nguvu sana, kiasi kwamba, mtu kuwa kama amepoteza ufahamu wa maeneo mengineyo ya kimaisha isipokuwa mapenzi tu.

Homoni hizi humfanya mtu kuwa na hisia za kuvutiwa na mwingine, uchangamfu, ukaribu, kuvutiwa na hisia za ukamilifu zaidi. Wale waliowahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi kabla ya ndoa au wale waliowahi au wanaotoka nje ya ndoa zao kwa kuvutwa kimwili na wapenzi wengine, wanajua inavyokuwa.

Lakini homoni hizi, hatimaye huanza kupungua na mtu huanza kuhisi kwamba alikosea. Huoni tena na huhisi kama ilivyokuwa awali. Sasa haoni kuwa mpenzi wake ni mzuri au anafaa kama iivyokuwa awali. Kwa sababu, homoni zile zimeshuka sana, mwili unakuwa hauna maana tena.

Kwa bahati mbaya kile kilichokuwa kinaitwa upendo, kilikuwa kimefungiwa kwenye mwili na homoni hizo ambazo kwa sasa hazipo. Hivyo, wapenzi hawana kingine cha kushika ambacho, wataweza kukiita mapenzi.

Unajua sasa ni kwa nini, tangu kale kabisa suala la wachumba kukutana kimwili kabla ya ndoa lilikuwa likipingwa sana? ni kwamba, watu wanapokutana kimwili, uwezo wa kukaguana tabia unakuwa umefungwa kutokana na kufumuka kwa homoni hizi, ambazo hubadili hali ya mtu na hisia zake kwa ujumla.

Kwa nini unadhani watu, hasa wanaume wakishaanza mapenzi ya kimwili na mtu mpya, yaani nyumba ndogo au yeyote, inakuwa rahisi sana kwao kujisahau na kukamatwa? Sababu ni hiyo hiyo, kwamba, uzalishwaji wa homoni hizi huwa ni mkubwa kiasi cha mtu kuamini kwamba, hakuna kingine chene kufurahisha na kuliwaza kama uhusiano huo.

Kumbuka, watu wawili wanapovutana, kwa maneno mengine tunasema kuna kemia kati yao. Hii ina maana kwamba, huwa kuna mabadiliko ya badhi ya homoni kama nilivyosema. Lakini,

wanapokutana, homoni hizi huwa nyingi kiasi cha kufanya upofu wa muda. Unaweza kuwa upofu wa mwezi, mwaka au miaka.

Upofu huu unapo malizika, uhusianao huwa ni wa vurugu tupu, kwa sababu kama nilivyosema awali, hqakuna mahali pengine pa kushika siyo tabia, mienenfo waa haiba.

Upofu huu unapomalizika, uhusiano huwa ni wa vurugu tupu, kwa sababu kama nilivyosema awali, hakuna mahali pengine pa kushika siyo tabia, mienendo wala haiba.

Inashauriwa kwamba, mtu anapovutiwa na mwingine au watu wanapovutana ni vema wakawa wangalifu sana. kwanza, wajue kwamba, uhusino ambao msingi wake ni miili tu, yaani tendo la ndoa haudumu, kwani homoni zitokanazo na kukutana watu kimwili, hazina maisha, huwa zinaisha haraka.

Lakini pia inashauriwa kwamba, mtu anapoingia kwenye mapenzi ajaribu kushariana au kuukagua moyo wake, akili pamoja na hisia zake. Kuacha tu mabadiliko ya hali ya mwili yakatawala ni kutafuta maumivu.

Hebu jiulize, ni kwa nini mapenzi yanapoanza kwa moto sana, huzimika haraka au kwa kishindo sana? ni kwa sababu yanajengwa kwenye msingi usioaminika, yaani katika mihemiko na kimapenzi. Penzi linalokua polepole ndilo lenye kushika, kwani halina msingi wa mwili.


Usisahau kushare post hii.πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome

Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU