-->

TUZUNGUMZE MWANAMKE🙇🏻‍♂

Image may contain: 2 people, people sitting
Je unataka NDOA kwa uhalisia upi? Maana NDOA inawahusu wawili Yaani MWANAUME NA MWANAMKE...
Ikiwa wewe umedhamilia kuwa na NDOA imara je mwenza wako umeipima dhamira yake? Maana kwenye akili ya Mtu Kuna MIPANGO lakini pia kwenye MOYO wake kuna UTASHI hapo unagundua kwamba ikiwa MWANAUME ATAKUJA KWAKO KWA MIPANGO maana yake huwezi kuwa na MUME utabaki na Mwanaume, Na ikiwa MWANAUME huyo atakuja kwako na UTASHI Dada umejikomboa maana yake UMECHAGUA KUWA NA MUME💪🏽
Kwa sasa ni rahisi sana kupanga MIPANGO ya NDOA hata mkiwa kwenye daladala🚎
Japo ni NGUMU mno NDOA kudumu kwenye FAHARI
Wahanga wa NDOA ni wanawake kwa sababu wao huwazia zaidi FAMILIA tofauti na Wanaume, Mwanamke ikiwa unawaona mashoga zako wanapendeza kwa NGUO nzuri siku ya NDOA zao, Jichange ununue gauni 👗 pamoja na viatu👠 kama ni picha nenda popote ukapige picha🤳🏼
NDOA ni safari yenye SIRI nzito tena iliyojaa GIZA.
Kuijua dhamira ya mwenza wako ni FUMBO pengine ukajua kupitia HISIA ila naomba nikwambie hakuna TESO GUMU KWENYE NDOA KAMA HOFU kwamba muda wote hujiamini wala hujui uko upande gani kwa mwenza wako, Yanini kujitaabisha kwa mambo ambayo wewe mwenyewe unaweza kuyatimiza ikiwa utajiwekea malengo😎
Usiifanye NDOA kama FASHION kwamba kwa wakati huu na toleo hili lazima ninunue
Furaha ya NDOA inaweza kukomea siku ya KUFUNGA NDOA ama ikaishi nanyi ikiwa mwenza wako atasimamia FURAHA YAKO lakini ikiwa haitakuwa hivyo niamini NI HERI KUFA BILA NDOA KULIKO KUINGIA KWENYE NDOA KWA MTU AMBAYE HAJUI MAANA YA NDOA😭
Mateso ya NDOA huwaka kama MOTO uwakao kwa bahati mbaya, Mzimaji hawezi kuwepo zaidi moto ule utateketeza kila kitu, Funga NDOA na MOYO WAKO kuliko KUFUNGA NDOA na AKILI YAKO maana akili inatabia ya KUDANGANYA🙋
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria💃
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU