-->

Thamani yako HAIPUNGUI kwa sababu watu hawathamini ama kukubali unachofanya.


Thamani YAKO inapungua pale ambapo UNAACHA KUFANYA kitu unachojua ni MUHIMU kwa maisha yako na ndicho Kitu SAHIHI kwa kisingizio kuwa WATU HAWAKUTHAMINI.
Hapo unajishushia thamani.Kuna mambo 3 unatakiwa kuzingatia:
.
1)Kuna watu HAWAKUTHAMINI kwa sababu bado hawajajua thamani yako lakini hiyo haimaanishi wewe hauna thamani.Njia nzuri ya kushinda hili ni kuendelea kufanya kwa ubora wa hali ya juu hadi wanaodhani unabahatisha Wajue kumbe ndio ulivyo.
.
2)Kuna watu hawakuthamini kwa sababu wanaona unachofanya wanatamani kufanya ila wameshindwa,hivyo wanataka kukukatisha tamaa kwa kukuonyesha kuwa unachofanya hakina thamani.
.
3)Kuna watu hawakuthamini kwa sababu wanaona haustahili.Duniani kuna maajabu ya watu kufikiri kuwa kuna watu wa aina fulani ndio wanahaki ya kufanikiwa katika mambo fulani.Kama wewe sio mmoja wa kundi hilo,ukianza kufanya wataonyesha kutokukuthamini.Hata Yesu alidharauliwa kutokana na mji aliotoka ulikuwa mdogo-
“Hivi jambo JEMA linaweza kutoka NAZARETI”.Walisahau kuwa thamani ya mtu haitokani na UKOO WAKE,ELIMU,KABILA ama MJI anaotoka bali UWEZO ALIONAO.Na wewe “
.
Kumbuka thamani yako haiongezwi kwa KUBISHANA ama KUSHINDANA na WASIO KUTHAMINI bali kwa KUENDELEA KUFANYA BILA KUCHOKA vitu vya THAMANI.
.
NAKUKUMBUSHA KUWA WEWE NI WA THAMANI SANA.
Image may contain: 1 person, close-up
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU