-->

ACHA KUJITESA Simanzi hutawala siku zote


.Mara nyingi hutokea baada ya mtu KUPITIA maumivu Makali ya KUPOTEZA mtu aliyekuwa anampenda sana,Kufanyiwa UBAYA mkubwa ambao hakuutarajia na bado haamini kama imetokea,Kupitia hali iliyosababisha UCHUNGU mkali Moyoni na ameshindwa KUSAMEHE n.k
.
Mtu anayepitia hali hii kila anapoamka asubuhi anakuwa na sababu nyingi za kuwa na huzuni,kulalamika na kutokuwa na furaha kuliko kufurahia maisha.Kuna watu wameruhusu hali hii iwatawale kwa miaka mingi na wengine imewasabababishia hadi magonjwa na imefupisha maisha yao.
.
Ni muhimu Kutambua kuwa wewe sio peke yako umepitia hali hiyo,wapo wengi walipitia na wengine wanapitia kwa sasa.Wengi wakipitia hali hii huwa wanaona kama ni wao tu ndio wanapitia,wanaona wana bahati mbaya,Mungu hawajali na Dunia imewageuka-Kumbuka kuna wengi walishinda na wewe pia unaweza kushinda.
.
Usikubali kuweka kisasi kwa mtu,Usikubali kubakia na uchungu ama hasira za ndani.Fanya maamuzi ya kusamehe hata kama aliyekusababishia hali hii hajaomba msamaha,ni kwa faida yako.Wengine ni wao wenyewe hawajajisamehe,Jitangazie msamaha.
.
Tambua bado una fursa ya kuishi MAISHA yenye furaha bila kujali maumivu uliyopitia,ulichopoteza ama mabaya uliyotendewa.Amini katika UKURASA MPYA wa maisha yako.
USIFUNIKE tatizo bali amua kulikabili kwa kulishughulikia mwenyewe ama kutafuta mtu wa kukusaidia.
.
Leo amua kufungua ukurasa mpya wa kuishi maisha ya furaha,”
Uliachwa na mpenz au ulimuacha bas unaa uhuru kuanzisha na mtu mwingine.. Bado wapo wenye nia ya kukupenda kwa dhati
.
Image may contain: 2 people, people dancing and people standing
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU