USITESEKE
Kuna wakati tunahisi tupo na wenza walioandikwa kwa maisha yetu na kumbe tunajivika UPOFU KWA MAHABA TUNAYOPATA KUTOKA KWAO, hali ya kuwa ndani yao ni walaghai na wasio na upendo.*
: *Kwa wakati ambao utakuwa unapitia maumivu makali ya kuachwa, basi JIKANE KWA WAKATI yaani jikatae kwamba sio wewe uliyempenda Mtu asiyekupenda.*
*Mwache aende na kama aliandikwa kuwa wako BASI MUNGU ATATENDA MUUJIZA ILI ARUDI na ukiona hajarudi kwa wakati ambao ndo ULIHITAJI ARUDI basi ACHILIA MAZIMA kwani asije kurudi na MAJANGA.*
*Mara nyingi vita vya NAFSI pamoja na MOYO vinapiganwa sirini, hivyo basi usisumbuke kupaza sauti kuambia watu MAGUMU UNAYOPITIA KWENYE MAHUSIANO YAKO kwa sababu kila mmoja na fikra zake.*
Kuna ambao wataona kwako itakuwa msaada kuachana nae, kuna ambao wataona hasara yako kutokuwa nae japo hawa ni wachache sana na pengine ndo wanaoweza kuupa TUMAINI moyo wako.*
*Unapoitafuta FURAHA YAKO usijaribu kumshirikisha mwingine, hulka ya binaadam ni WIVU.*
Mtu asiye sahihi haogopi kukuacha bali anakuwa nawe kwa wakati autakao yeye, iwe kwenye mahusiano ama ndoa, akishaona humfai tena wala hatajiuliza mara mbili.*