-->

NIKO NJIA PANDA NAOMBENI USHAURI WENU

Black couple standing under coat trying not to get wet Stock Photo - 33805998

Niko kwenye mahusiano na mwanamke ambaye nampenda na Mungu akipenda mwaka huu tunafunga ndoa, lakini pia kuna mwanamke mwingine ambaye nilikua naye tangu nikiwa chuo. Tumekaa kwenye mahusiano kwa miaka 8 (huyo mwingine), katika kipindi chote hicho amekua akipata ujauzito namuambia atoe, ametoa mimba zangu 4, tumekua tukiachana na kurudiana na sababu kubwa nikuwa mimi nina mtu wangu lakini huyu dada ana nyota flani, kila nikiwa naye huwa Napata pesa sana.
Mimi ni wakili, nina kampuni yangu, sifanyi kazi naye ila ni mtu ambaye ananipa michongo mingi, ana mawazo mengi ya akili, anakushauri vitu vingi vya maendeleo. Wazo lako la kawaida anaweza kulifanya kuwa kubwa sana. Mwaka jana mwishoni tuliachana, aliniambia niende kwao kujitambulisha, nilimuahidi kwenda lakini mwisho niliona hapana, mchumba wangu alipata ujauzito nikaamua kwenda kwao kujitambulisha na kutoa mahari. Yeye hakujua kama nimeenda sehemu nyingine kujitambulisha ila alikasirika kwakua nimemdhalilisha kwani waliita mpaka ndugu.
Niliomba msamaha sana lakini alikataa katakata, mwisho nilikubaliana na ukweli na kuamua kuachana naye nikijua kuwa atarudi ila mpaka mwezi huu alikua hajanitafuta. Niliamua kumtafuta ndipo niligundua kuwa kuna mwanaume anaishi naye na ana mimba yake. Hawajafunga ndoa bado, nilimfuata na kumuomba msamaha ili angalau tuwe marafiki lakinia ligoma na kuniambia kuwa sasa hivi ana mtu wake. Nilituma watu nikalia mpaka akanikubalia, nadhani wameachana na mtu wake.
Sasa baada ya kuachana na mtu wake amekuja kwangu anataka nimpeleke kwetu kwanza nikajitabulishe ndiyo twende kwao, nimechanganyikiwa kwa kweli, nimemuambia twende kwao kagoma, ishu inakuja kuwa kwetu nina mchumba na nakaribia kuoa, angalau angekubali niende kwao ili nivutevute muda hata nioe kwanza ndiyo baadaye nimuombe msamaha nimue mke wa pili. Lakini shida nyingine nikuwa ana mimba ya mwanaume mwingine, sasa hapa nitaishije naye wakati tayari sasa hivi mtoto mwenyewe hata kabla ya kuzaliwa nishaanza kumchukia?
Natamani tuachane naye tu tuwe marafiki ila nashindwa nimeshajichanganya kwani kule nako kashaachana na Baba wa watoto wake hawaongei kwani kamuambia mimba si yake ni yangu? Nashindwa namna gani hata nitamuacha tena bila kumuumuza, sijui nifanye nini?
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU