-->

TATIZO LA KUPOTEZA HAMU YA KULA WAKAITI WA UJAUZITO NA TIBA YAKE

Baadhi yetu hupoteza hamu ya kula kipindi cha ujauzito,,, jambo hili ni baya sana kwa vile mama mjamzito anahitaji apate chakula cha kutosha ili mwili uweze kufanya kazi zake kiufanisi, anatakiwa pia ale kwa wingi mboga za majani hasa matembele na mchicha ambayo yanaelezwa kuwa yanaongoza kwa kuongeza damu.
Mwanamke wakati wa kujifungua hupoteza damu nyingi hivyo lazima ale chakula cha kutosha pamoja na mboga za majani na vitoweo kama samaki, nyama n.k
Sasa inapotokea mama mjamzito akawa hana hamu ya chakula msimuache tu na kusema .... ni mimba inamsumbua.... Hilo ni tatizo na mnapaswa kulichukulia hatua ili kumpa mjamzito afya njema, leo ninakukumbushs tips hizi ziwasaidie kumpa mjamzito hamu ya kula.
1. KUNYWA MAJI YA MACHUNGWA
~Mama mjamzito atengeneze juisi ya maji ya machungwa kiasi cha lita moja, kisha awe anakunywa glass moja moja kila baada ya muda fulani katika siku hadi itakapomalizika
Hii itamfanya awe na hamu ya kula vizuri na itakapomtokea tena ile hali ya kutotamani chakula basi na atengeze tena na kutumia kama hapo juu.
2. HABBAT SAWDA NA LIMAO
~Dakika kumi kabla ya kutayarishwa kwa chakula chukua kijiko kidogo cha unga wa habbat sawda koroga kwenye glass ya maji au/juisi na weka maji ya limao kiasi cha kijiko kikubwa humo kwenye glass na unywe, baada ya muda mfupi utajiskia hamu na utatamani msosi usichelewe kufika mezani.
Hapo sasa jitahidi kula chakula cha kutosha zikiwemo mbogamboga nilizozitaja hapo juu pamoja na matunda kama papai, parachichi, nyanya, fenesi, machungwa na aina zingine za matunda yanayoweza kupatikana.
Pia kwa mama mjamzito sio lazima awe na milo miwili kwa siku, anaweza kula hata mara sita kwa siku. Kula kidogo kidogo mara kwa mara umfanya kuwa na nishati nyingi zaidi kwa afya yake na mtoto aliye tumboni.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU