Sikia π nikuambie
Alipokuonyesha upendo ulimweleza Kila mtu wa karibu habari zake tena ukapost na mahaba yenu mitandaoni.
Ukaamini kuwa ndiye sukari wa maisha yako nasi tukakupongeza na kukuombea kama ulivyotuomba.
Ulipoelezwa Mabaya yake ukaziba masikio hukutaka kusikia ya watu kwa kuwa uliamini mtu aweza haribu mahusiano yenu, naam, ulifanya vyema.
Japo unatakiwa kutopuuza kila unachoambiwa na watu,fanyia kazi.
Japo unatakiwa kutopuuza kila unachoambiwa na watu,fanyia kazi.
Leo umejionea mwenyewe maovu yake unaanza kulia na kupost post za kuumizwa na kuhitaji tulizo kutoka kwa marafiki wa fb,WhatsApp na Instagram kulaani mapenzi na ndoa.
Ndugu tafakari Kuna wakati Mungu huinua watu wa karibu yako kukuambia ukweli juu ya mwenzi wako.
Kumbuka hili si Kila akuambiye ukweli juu ya mwenzi wako Ni adui wa penzi lako....
Sometime unahitajika uchunguze mwenyewe na upatapo jibu Basi jiepushe mapema usije pata maumivu ya kudumu ya moyo na ukamkosa wa kukutuliza maradhi yako.
Naimani umenielewa na Kama hujanielewa Basi huu ujumbe si wako Ni wa yule kuleee.
Imeisha hiyo....