-->

MAUMIVU NA KIDONDA CHA MAPENZI HUPONA KWA KUFANYA YAFUATAYO...

Image may contain: one or more people, sky, outdoor, nature and water
Nafsi haiwezi kujua kosa mtu alifanyalo kwani haijui kuwaza hayo, Nafsi kazi yake ni KUPENDA... Mambo ya chuki, hasira na ubaya wowote ni kazi ya akili, Kinachohangaisha wengi kwenye Mahusiano ni KUMBUKUMBU! Kinacho chelewesha FURAHA baada ya kuumizwa ni zile kumbukizi ambazo mtu anazo ndani yake, Kuziacha kumbukumbu ambazo ulizijenga mwenyewe ni kujidanganya, Japo zinatesa lakini hilo ndilo penzi ambalo linaweza kutajwa Moyoni mwako, Unaweza kuziacha kumbukumbu hizo zibaki peke yake lakini ukajitengenezea kumbukumbu mpya ili ujitenge na UPWEKE... Kutengeneza kumbukumbu MPYA ni rahisi ikiwa utakuwa huna kumbukumbu zingine JE UNAWEZA KUONDOKA KWENYE KUMBUKUMBU ZA AWALI KWA KUPANGA?
Usijidanganye rafiki yangu kilichomo ndani ya nafsi hakiondoshwi kwa kupanga bali kitaondoka kwa nafsi kuchoka kuhangaika, Kama huwezi kukubari usiwe na masalia ya kumbukumbu za kale basi usijaribu kutengeneza kumbukumbu mpya maana utakuwa unajiongezea matatizo ya ki fikra, Unakijua kinachokuijia zaidi kichwani mwako juu ya huko unakotaka kutoka? Kama unakijua basi hicho ndicho kinakugharimu, Mapenzi yakiisha hayawezi kuendelea bali yanaweza kuwepo kwa mitazamo ya wahusika, Mapenzi yanalenga nafsi na ikiwa nafsi iliisha kuwa nyeusi basi usilazimishe mwisho wake mbaya, Tengeneza yaliyo na utulivu ki akili na nafsi ipokee ili uweze kuwa mahala salama, Kulazimisha mtu akupende ni KUJITAABISHA na mwisho kabisa utajikuta unaangamia kwa kukosa utulivu wa mawazo.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU