Kwani kwenye maisha tunajua kwamba kuna wakati wa kufurahi na wakati wa majonzi, Majira hayo yaliwekwa na MUNGU ili kutupa kusahau nyakati MBAYA NA NZURI
Lakini yanapokuja magumu yanatujenga, Na yakija Mema yanatujenga pia, Hayo ndo MAISHA YA VIUMBE WOTE.
Lakini usijaribu kuliacha pendo lako bila kuwa umelipigania, Kwamba umebaini MWENZA wako hana malengo nawe, Hapo unaweza KWENDA.
■ Dada akatoa chozi na kusema LAITI KAMA MUNGU ANGELIKUWA NA OFISI DUNIANI SIJUI KAMA MATATIZO YANGU ANGEYASUBIRISHA! Nimeteseka sana na Mahusiano pamoja na ndoa yangu, Nimelia nikanyamaza mwenyewe, niliugua nikajitibisha mwenyewe, Nilitaka kujiua nikajiokia mwenyewe lakini ambaye amekuwa akisababisha hayo wala hakujali zaidi aliniacha na wala hakuja kutaka kujua kilifuata nini baada ya hapo😭😭
Lakini Elista Mimi sina tatizo juu ya kuachwa ila kinachoniuma Kwanini anaamua kutaka kuniacha kipindi ambacho Bado NAMPENDA?
■ Pole sana rafiki yangu, Kwanza nikupe HONGERA UNA MOYO JASILI💪 na kama hujafa mpaka leo huwezi kufa kwa MAPENZI ila ninachojua ni kwamba MUNGU YUPO UPANDE WAKO!
Lakini Tina natamani kujua tatizo lililopelekea mkafikia hali hiyo ambayo wewe kwa upande wako imekukosesha tumaini, Ninaweza kupata mawasiliano ya Mwenza wako japo kwa ufupi nimsikilize?
■ Elista namba zake nakupa nae akwambie ya kwake;
0800 543210☎
■ Kwakuwa nimechukuwa jukumu la kumsaidia Tina niliinua simu☎ kupiga kwa MWENZA wake, Simu📞 ilipokelewa na nikajitambulisha kama msamalia mwema ambaye nimemkuta mkewe mahala akitaka kujiua kwa kumeza vidonge, Majibu yake yalikuwa kama ifuatavyo;
■ Kwanza Kaka pole sana kwa kazi ambayo haikuhusu, Tuna wazazi pande mbili, Tuna mshenga pamoja na kanisa kulikuwa na haja gani kudhihilisha ujinga wake kwako?
■ Ndugu yangu Mimi kama bin adam siko tofauti na mshenga, mzazi, ndugu, rafiki, mchungaji ama shekhe ama mtu anaeijua ndoa yenu, Mimi nimewiwa kuongea nanyi na kama hutajali naomba tukufuate ulipo ama wewe utufuate hapa NYERERE SQUARE.
■ Basi nakuja hapo baada ya DAKIKA 20.
■ Asante kaka kwa heshima UMENIPA.
Baada ya kukata simu nikampa mrejesho TINA nae akafurahia hali ya
Mumewe kuitikia wito wangu maana walikosa maridhiano kiasi kwamba kila mmoja alipita njia yake na wapo nyumba moja.
■ Elista Asante sana! Yaani mimi naomba tu hata kama hanitaki Basi asiniache kwa ghafla NITAKUFA MIE KWANI NAMPENDA ila kama ataniacha taratibu itanisaidia nami kuanza kuji-cancell taratibu japo najua itanigharimu😭😭
■ Maneno ya TINA yaliniumiza sana kiasi nikajikuta naingiwa huruma ya ajabu, Moyoni nikajiuliza HIVI HUYU JAMAA ANAJUA KAMA ANAPENDWA KIASI HIKI?
Mwisho nikajisemea Amaa kweli PENYE MITI HAKUNA WAJENZI.
Nainua kichwa namuona jamaa akitembea kuelekea tulipokaa ndipo Tina akasema ni Mumewe, Karibu sana kaka.
■ Asante bro! Ndo Mimi uliongea nami kwenye simu, Naitwa Peter ndiye MUME wa huyu Mwanamke, Na nimeitika wito ili nijue Kwanini wewe kuingilia MGOGORO HUU?
Kaka Huyu Mwanamke ni Mke wangu ila ninaloweza kusema kwa ufupi sana ni kwamba TINA ANA KIBURI na anatabia ya kununa bila sababu ndo maana tunapotofautiana hawezi kushirikisha ndugu zangu wala wake kwani anajijua hawezi kupata wa kumkubalia anivunjie heshima Mimi, Lakini pia Tina mkigombana hawezi kutoa huduma yoyote kwangu na Mengine wala Sina haja ya kusema hapa, Na labda niseme kwamba HUYU MWANAMKE HAKUPATA ELIMU SAHIHI YA MUME ndo maana hatuishi kugombana, Naomba nikomee hapo.
■ Peter nimekusikia vizuri na hapa nimegundua tatizo lenu ni DOGO ila linayo madhara MAKUBWA kama hamtajua kuenenda na wakati wa NDOA yenu, Kwamba UPO TAYARI KUPOTEZA MKE KWA SABABU ANANUNA SANA? Peter mkeo anakauli mbaya ndo huwezi kumjenga abadilike? Na wewe Tina Mumeo unataka kuachana nae kwa sababu ni mbabe?
Mimi mtanisamehe hapa nilichokiona ni kwamba NINYI NYOTE NI WATAWALA😂😂
Kwamba kila mmoja anataka mwenzie awe chini yake, Ila Tina wewe ni MKE huwezi kumshusha Peter awe chini yako, Lakini unaweza kuishusha temper ya Peter mnapokuwa MMETOFAUTIANA.
Peter ni kweli unaweza kumtawala Tina ni haki yako ila ninaloweza kukwambia KULIKO KUMTAWALA KWA MADARAKA YA KIUME ni busara sana kama ukimtawala kwa HEKIMA.
Tina msamehe Mumeo na UMTII Kwani ukimtii huwezi kupambana nae, Peter naomba sana rudisha moyo wako kwa Mkeo Kwani Mimi ni Mwanaume MwenZio TINA ANAKUPENDA ATAKUPENDA DAIMA Kwani pamoja na yote still TRUE LOVE YAKE IPO KWAKO.
Baada ya kusema hayo nawaombeni sana mfikirie kwamba mpo kwenye NDOA na kama mliunganishwa na MUNGU basi MUOGOPE laana ya MUNGU Kwani anachukia KUACHANA isipokuwa kwa UZINZI na kwenye kesi yenu sijasikia usaliti na kama Kuna ambaye anachepuka maana yake ANAZINI NIMUOMBE AACHE MARA MOJA Kwani mpaka sasa unaficha mwenzio hajui ila iko siku MUNGU atakuumbua, Baada ya kusema hayo nawaomba mshikane mikono mbele yangu na MTAMKIANE MSAMAHA👏
■ Elista Asante sana kwa kipawa MUNGU amekupa, Kufikia hapa MKE WANGU NIMEMSAMEHE na kwa hakika Kuna ambayo nimeyahifadhi ndani yangu, Kaka huyu ni Mke wangu japo nilianza kukata tamaa ila naomba nitamke kwamba TINA ULIKUWA UNANIUMIZA SANA ndo maana niliamua kukupuuza ila MSHUKURU MUNGU aliyekukutanisha na Elista kwa hakika ANAYO NGUVU NDANI YAKE nikiri nimekusamehe MAMA.
■ Peter Mume wangu kwa udhaifu, ujinga ama kujifunza upumbavu hata nikaiweka rehani ndoa yangu NAJUTIA BABA😭😭
Nisamehe MUME wangu sirudii, Yaani nimejiona mjinga sana kwa makosa ambayo yangeivunja NDOA yangu😭😭
Sintorudia Baba naomba niamini Mume wangu.
■ Mr and Mrs Peter niseme MUNGU ANA MALENGO NA NDOA YENU msikubari NDOA yenu ikafa kijinga kiasi hiki, Makosa ama makwazo hayana budi kuja ili kuwajenga, Na mkiona NDOA yenu iko na AMANI muda wote bila migogoro Kuna UPANDE UNA UNAFIKI Sina maana nahitaji migogoro ila ninachoweza kusema ni kwamba MIGOGORO IKISAHIHISHWA HUJENGA DHAMANA MOYONI hivyo mjitathimini na MUNGU AWASAIDIE
Baada ya kusema hayo Mimi niseme kwamba;
NDOA ama MAHUSIANO mengi yanakufa kwa sababu ya kutoongea, Peter mkeo hakuwahi kujua kinachokufanya umpuuze, Tina kujinunisha na kujibu utakavyo kwa Mumeo wala hakuwahi kujua kinachokufanya uwe hivyo zaidi kila mmoja alitaka kunyenyekewa, Na kumbe majibu ya tatizo lenu ni haya;
MAWASILIANO HAYAKUWA HAI japo mliendelea kutunishiana misuri but UPENDO WA DHATI SIKU ZOTE UNASHINDA na hapa nimeuona USHINDI wa pendo lenu, Niwatakie MAISHA MEMA YA NDOA ikimpendeza MUNGU atimize maono ya NDOA yenu👏🏼
■ Elista tunakushukuru sana MUNGU WA PETER NA TINA AKUBARIKI SANA tunakukaribisha kwenye MAISHA yetu uwe rafiki yetu kwa hakika hatukuweza kumpata mtu wa kuiponya NDOA yetu na nikiri ILIKUWA UKINGONI.
■ Asanteni sana na MUNGU AWATUNZE👏
■ Ndugu msomaji wa MAKALA hii ikiwa unapitia changamoto ya mahusiano ama ndoa kwa aina ya TINA NA PETER angalia zaidi madhaifu yako kabla ya ku-judge ya mwenza wako, Hakuna bin adam aliyemkamilifu sote ni WADHAIFU.
Maongezi, Mawasiliano, pamoja na Heshima hayo ndiyo ambayo yanaweza KURUDISHA UPENDO ambao ulikuwa unaelekea kufa ama umekufa, Siku zote nature ya MAPENZI ni upendo na kama ndivyo KWANINI UKUBARI UPOTEZE PENDO LAKO?
Nzi🐝 anafia kwenye kidonda kibichi hiyo ni hukumu ya mwenye kidonda, ukiona nzi🐝 anafia kwenye kidonda kikavu ujue SIKU ZAKE ZILIKUWA ZIMEFIKA😂😂
#Elista_Kasema_ila_Sio_She