Kwanza kabisa kipimo kikubwa kwenye Mahusiano ni pale unapokuwa mbali na mtu ambaye unampenda kwa moyo, Muda pamoja siku kuwa nyingi bila kumuona UMPENDAYE ziko athari kuu mbili;
1. KUMSAHAU.
2. KUTOMPA KIPAUMBELE.
Bin adam yeyote huishi kwa MAZOEA... Yako matukio mawili makubwa ambayo hubeba taswira ya penzi, Kwanza kabisa SIKU YA KWANZA KUKUTANA NA MTU NA UKASEMA UMEMPENDA lakini jingine ni WAKATI AMBAO ULIFURAHIA NA MWENZA WAKO! Mara nyingi kwenye taabu huwa hatukumbuki sana laa kama ni nje ya Mapenzi, Kwenye Mapenzi taabu huwa hazina nafasi kwenye akili ya mtu ila nyakati nzuri, Ukiona mtu anakukumbushia nyakati mbaya ujue MOYO WAKE HAUKUHITAJI TENA... Ndo maana nikasema mambo mazuri ya kale ndo hubeba kumbukizi nzuri za Mapenzi, ukiwa mwelewa ANZA SASA KUJENGA MAMBO MAZURI KWA MWENZA WAKO ili hata akikengeuka na kukuacha akaishi kwa mateso baada ya kukosa PENDO LA MOYO ambalo kwako alilipata, Nikwambie jambo moja UPENDO WA DHATI haupatikani kama mahindi yanayomwagika sokoni ila unapatikana kwa GHARAMA YA AKILI, MUDA, MOYO pamoja na KUJITOA! Wengi wanalia kwa kukosa mtu sahihi lakini mwisho wa siku inawabidi kuyaishi mapenzi kwa sababu ya MAZOEA ama mtu kuona hana mbadala, Jifunze kuubeba uhalisia wako ili ukuongoze kwenye safari ya MAPENZI... Mapenzi sio kama mchezo wa KUBET ila ni ajira, Maana yake unalo jukumu la kusimama kama MWAJIRIWA ili ujue ufanisi wako katika penzi lako, Usijaribu kumpuuza UMPENDAYE maana utakuja kujutia akikuacha, Mapenzi yanataka UWAJIBIKAJI.
#Elista_kasema_ila_sio_She