-->

Kwanini MAPENZI YA SIKU HIZI YAMEKUWA MWIBA WA MOYO?

Image may contain: 2 people, people sitting
Kwanza kupenda ni agizo la ALLAH... Kinachowachanganya watu wameyabeba MAPENZI kuwa sehemu ya KUBURUDISHA NAFSI ZAO na sio kuhurumiana, Ukimpenda mtu lazima uwe na huruma nae na huko ndiko utautaja UPENDO WA DHATI! Ukimtazama mtu kwa muonekano wake ni ngumu kumpa hakika ya kumpenda kwa sababu moja tu NGUO ZINAVULIWA na uhalisia unaonekana kwa utupu, Wengi wamekuwa walevi wa mionekano ya WANAWAKE/WANAUME na hilo ndilo limesababisha MAPENZI kukosa sura halisi, Ndo maana mimi enzi zangu nilimtafuta shemeji yenu asubuhi hata mswaki hajapiga, amejivalia kanga na T'shirt chakavu, Lakini ukitaka kumpata Mtu umtaje katika upendo na amejikoki kwa unadhifu UTAKUWA UNAJIDANGANYA MWENYEWE... Naomba nikwambie na unielewe UPENDO heshima yake udumu kwa matendo manyoofu, Lakini ukiisha ji-tune kwa MUONEKANO kwamba huo ndo unakufanya umpende mtu utakuwa unajichemshia maji moto mwisho wa siku utalia, Yajenge Mahusiano/Ndoa yako kwa UPENDO WA HISIA wala usijaribu kumpa nafasi mtu ambaye ANAKUVUTIA KWA MUONEKANO WAKE... Kuna wakati Muonekano unatoweka kwa mazingira pamoja na mabadiliko ya maisha, Baada ya kusema haya naomba nisisitize tena MPENDE MTU AMBAYE ANAUFANYA MOYO WAKO UWE MTULIVU.
#Elista_kasema_ila_sio_sheria
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU