-->

KWANINI HURIDHIKI MKE WANGU?

Image may contain: 2 people
Kauli ya kujiamini ikitoka kwenye kinywa cha Mr Hamad, Yalikuwa maneno machache lakini yalijaa lawama ndani yake, Kwa uchungu Mwanamama Janeth akalia sana, Uchungu wake sio kwa sababu ya kile ambacho alikuwa akilalamikia ambacho hicho ndo kilimtoa kauli ile mumewe, Alilia kwa kauli ya mume wake kwani Mumewe alidhani kinachomliza mkewe ni kwa sababu ameonyesha kutoridhika kwa mengi mazuri ambayo alikuwa akifanyiwa na mumewe... Mume wangu maisha ya ndoa sio kunitimizia mahitaji tu bali nahitaji lugha nzuri zenye kunijenga ki mapenzi, Nisemeshe maneno ya upole Babaangu, Nionyeshe kwa matendo ya upendo kuliko kudhania ufanyayo eti chakula ama tendo la ndoa hayo ndo yanaweza kuutuliza moyo wangu, Kama Mwanamke nahitaji KUPEWA KIPAUMBELE CHA AMANI ili nijisikie kweli niliwaacha wazazi wangu na kuambatana nawe ili nafsi yangu ipate tulia Baba, Hamadi akiwa mwingi wa mshangao alijikuta anatokwa na machozi, Maneno ya mkewe yaliubomoa ubongo wake na kuanza kuwazua mambo kede kedee, Alifikiria kumbe MKE WA NDANI HATA AKIPATA KILA KITU LAKINI AKAKOSA MANENO YA KUUFURAHISHA MOYO NI HATARI? Nimekusikia Mke wangu, Natamani kama maneno uloniambia ungesema wakati hata hatujagombana, Ni wewe Mume wangu ndo hunipi nafasi ya kunisikiliza ili niweze kuelezea hisia zangu, Umekuwa ukiamini mimi sina tatizo lolote kwa sababu kila hitaji la maisha unalipa kipaumbele lakini Mume wangu yote hayo ni mema sana ikiwa utanipa huku nikiwa mwenye FURAHA NA AMANI! Lakini kama sina vitu hivyo ni bure Babaabgu, alimaliza Kuongea Bi Janeth na kumsogelea mumewe akaamkumbatia na kuanza kulia, Hamad akiwa hajui ajibu nini alijikuta akilia na Mkewe wala hapakuwa na mtu wa kuwanyamazisha, Mapenzi ni HAZINA YA UTU WEMA kila mmoja wao alitamani kusema ujumbe wa moyo wake ili kumjenga mwenza wake, Nimekusikia Mke wangu niseme jambo moja MUNGU NDIYE AKUJUAYE SIRINI vivyo hivyo MUNGU ANANIJUWA SIRINI... Hivyo niseme SINTOKUUMIZA TENA makosa yangu nimeyabaini wala sikuwahi kujuwa kama FURAHA NA AMANI ndo kila kitu kwenye Mapenzi na sasa nitamke nitakupatia haki yako Mamaangu, Nimekusikia Mume wangu binafsi nimesema ili uniponyeshe Mume wangu maana wewe ndo TABIBU WANGU! Sikuwahi fikiria kama unatatizo kubwa litakalonifanya nikuvunjie heshima, Mume wangu naomba tuhitimishe kwa kusema HAKUNA MWANAUME WA KULINGANA NAWE MOYONI MWANGU ndo maana nimekuwa nikikulilia unisikilize hisia zangu kwako, Asante kunipa sikio lako UMEUPONYESHA MOYO WANGU... Baada ya Janeth kufunga mjadala ule wawili hao wakakumbatiana na kuendelea na mambo ya kuzima taa, Mama nanihiii geukia huku.
Katika ujumbe huu liko jambo moja kubwa "MARIDHIANO NI UPONYAJI WA MAHUSIANO/NDOA" Kumsikiliza Mwenza wako ni uzima wa PENZI! Kila mkosaji akiweza kukubari kuambiwa ni rahisi kuepuka msuguano ndani ya penzi hilo, Mpe nafasi ya Kumsikiliza Mwenza wako ili yanayomtesa aweze kukuelezea, Ukiweza fanya hivyo KULINDA PENZI LAKO ila ukiona nakuchosha acha uje kuchutama ukimbembeleza Mwenza wako.
#Elista_Kasema_Ila_Sio_Sheria
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU