-->

KWANINI USIMKUBARI MWANAUME/MWANAMKE WA KULETEWA NA MTU?

Image may contain: 2 people, people smiling, people standing, outdoor and text
Mapenzi yanaweza kuota mahala popote na yakasitawi ikiwa wawili hao watajua maana ya UMOJA WAO... Hayupo mtu anampata mwenza wake kwa ndoto bali unaweza kuota taswira ya Mwanamke/Mwanaume fulani kwa sababu tayari Mwanamke/Mwanaume unayemhitaji amekujia ndotoni, Hakuna mahusiano yalopatikana kwa muujiza KILA MMOJA ANAPATA MWENZA WAKE KUPITIA HAJA YA MOYO WAKE KWA KUPAMBANA MWENYEWE! Sokoni ama kanisani/Msikitini ni sehemu inayowakutanisha watu lakini kila mmoja kwa juhudi yake anaweza kujichagulia mwenza wake, Ni kweli MAHUSIANO ni mwiba kwa sasa yaani kuna wakati mtu unaweza kuishi peke yako ukawa na Furaha tu tofauti na ukiwa na mtu, Ila asikwambie mtu MAHUSIANO ni faraja kubwa kwenye maisha ya bin adam hata wanyama nao kwa namna yao wanafurahia wawapo wawili, Uhitaji wa mtu kuwa na mwenza ni siri ya MOYO wake kwa namna ambavyo anamtengeneza mwenza wake kwa taswira, Usikubari Macho ya Mtu mwingine BABA, MAMA, DADA, KAKA na hata ndugu au jamaa kukutazamia Mwenza wa maisha yako, Iko hatari Moja MWENZA ANAYELETWA NA MAFIKIRIO YA WENGINE anaweza kukufaa kwa kusikiliza sifa zake lakini nikwambie wazi UPENDO WA KWELI UNAMBEBA MTU AMBAYE UMEMTENGENEZA WEWE KWA MACHO, AKILI NA MOYO WAKO KURIDHIA... Pengine ndugu, Jamaa au wazazi wako wanahitaji uwe na mtu wa aina fulani JE WANAUJUA UTASHI WAKO? Kuruhusu uwe na Mtu ambaye unaulazimisha moyo wako kuwa nae ni hatari sana, Unaweza kujikuta UMEZAA NAE bila kutarajia hicho ni kitanzi, Unaweza kujikuta UMEOA/UMEOLEWA nae hicho ni kitanzi, Madhara hayapo wakati huo ila baadaye akiishakuja mtu ambaye atagusa Moyo wako, ONE MISTAKE ONE GOAL🥅
#Elista_kasema_ila_Sio_sheria.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU