-->

KWANINI MOYO WA MWANAMKE NI MKUNJUFU?

Image may contain: 1 person, smiling, sitting, grass, tree, outdoor and nature
Jiuilize mara mia mia juu ya MOYO wa Mwanamke, Kwamba ndiye Bin adam pekee awezaye kukabiliana na MAUMIVU NA MWISHO AKASAMEHE NA KUSAHAU... Wanaume hatuko hivyo, Mwanamke akikuhesabia MATESO aliyopitia kwenye maisha ya MAPENZI lakini Bado anampa Mwanaume mwingine nafasi kwa kuamini kwamba HUYU HAWEZI KUWA KAMA YULE hapo ndipo utakubaliana nami kwamba MUNGU ALIMFANANISHA BIN ADAM MUME NA MKE KWA UBIN ADAM ILA SIO KWA MOYO! Moyo ulioko kwenye mwili wa Mwanamke UNA VIWANGO VYA TOFAUTI NA MOYO WA MWANAUME🙋🏻‍♂
Jiulize jambo moja tu ikiwa wewe ni Mwanaume unayejua MAPENZI YANAUMA... Ukimkuta Mpenzi wako "MWANAMKE" kwenye kitanda chako yupo na house boy UTAFANYAJE?
😂😂😂 Nacheka lakini Inauma aisee, Hilo tukio litazame kwenye vichekesho na movie tu ila usiombe likakukuta kwa kulitazama kwa macho yako😭😭
Lakini Mwanamke anao uwezo wa kushuhudia na akambebesha makosa house girl ili kuulinda MOYO wake💃
Kwa ufupi Mapenzi ndiyo kitu chenye maumivu makali kuliko kitu chochote kile laa kama HUJAPENDA NA UKAUMIZWA! Wanaume hatuwezi kuhimili Mkeo kutongozwa ije iwe KUMKUTA MAHALA AMECHUTAMA? Weeeee hapo ndo utajua hakunaga Mwanaume zoba kwa mkewe💪🏽
Tuwalinde Wake zetu kwa jambo moja tu "KUMPA SABABU YA KUFURAHIA UWEPO WAKO" Kwanza ijulikane DUNIA IMEPINDUKA YAANI JUU CHINI NA CHINI JUU Kwanini nasema hivyo? Kwa sasa Mtoto wakike ndiye mwenye shauku ya maisha kuliko Mtoto wakiume, Yaani WANAWAKE ndiyo walio kwenye KUPAMBANIA MAISHA KULIKO WANAUME hilo halijifichi, Kadiri siku ziendavyo WANAUME MTAJIKUTA NDO MNAJIPANGA KUJIUZA NA WANAWAKE WATAKUJA KUCHAGUA AMTAKAYE... Kwanini nasema hivyo?
Iko wazi kabisa KILA MWANAMKE KWA SASA ANAAMINI KWAMBA HAKUNA TENA MAZAO YA MUME ILA WANAUME! Kwahiyo itafikia mahala wanawake watataka Mwanaume kwa haja ya mwili na baada ya hapo kila mmoja asepe zake, Na hilo lilishaanza na kama Wanaume hatujakaa na kujisahihisha UKIMKOSA MWANAMKE ALIYEKUPENDA UTAPAMBANA NA KIAMA CHA KWENDA KUMTOA MTU JASHO JEMBAMBA💃
Ifike Mahala tuuhurumie MOYO WA MWANAMKE una mengi umepitia na hata lile zoezi la MP ni teso tosha kumfanya mtoto wakike kubakia IMARA MOYONI MWAKE... Tuwape wanawake kipaumbele kwenye kuwajenga kwamba SIO KILA MWANAUME NI MUONGO ili warejeshe IMANI japo kidogo kwetu.
#Elista_kasema_ila_Sio_sheria🔥🔥
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU