Maisha kila mmoja na NDOTO zakeπ
Kuna anae ota ndoto asubuhi, Kuna anae ota ndoto mchana, Kuna ambaye yeye ili aote ndoto lazima awe kwenye DALADALAπ
Lakini wote wanaota ndoto kila mmoja na vile anavyokuwa amewazia mchana, Usiku, Hata maeneo ya kazi ili mradi upitiwe japo usingizi mdogo HAPO NDIPO NDOTO ITAIBUKAππ»♂
Ukibahatika kumpata mtu aliyeota MAFANIKIO tangu akiwa mtoto HUYO ANAKUFAAπͺπ½
Ikiwa yale ambayo aliyapenda na kuyawekea maanani na alipokuwa mkubwa sasa anayaishi HUYO MSHIKEπ€πΌ
Kwa bahati nzuri zamani tulicheza michezo ya ujenzi wa FIKRA... na upo mchezo uliitwa BABA NA MAMA Maana yake ni ndoa ya mchangani, kwenye vichaka na nyuma ya tofari huyo KWANINI ASITAMANI UWE MKE/MUME WAKEπ€·π½♂
Mtu anaweza kuwa kikwazo kwako JE UNADHANI YEYE NI SHETANI KWAMBA BORA UMUACHE UKAMTAFUTE MALAIKAπ€·π½♂
Kwenye maisha unahitaji jambo moja tu;
"KUKUBALIANA NA KILE ULICHONACHO NA KUKIFANYA KUWA CHENYE THAMANI HATA KAMA HAKIKO KWENYE THAMANI UITAKAYO NIAMINI KITAKUWA KWA SABABU KIPO MOYONI MWAKO"
PENGINE hayuko kama wanaume/wanawake wa MATAIFAπ
Walivyo wao wanajua kuvaa, kumiliki majumba, Wao ni wenye muonekano pamoja na wingi wa MALIπ¬ππ¬π₯
YEYE ni MAJID/MARTHA tena mshamba kabisa, hawezi kufanana na wale maana wao ni wao na Yeye ni YEYEπͺπ½
Ukitaka awe kama MWANAUME/MWANAMKE ULIYEKUWA UNAMUOTA TANGU HAJABALEHE/HAJAVUNJA UNGO Mfanye Awe kama huyo, Hakuna shule katika kumbadili ili aendane na Mwanaume/Mwanamke huyo unayemhitaji bali ni YEYE KUENDANA NA WEWE N THEN AKUFANYE WEWE KUENDANA NA YEYEπHamuwezi kujenga furaha ya PENZI lenu ikiwa muda mwingi mnautumia kwenye kusuruhisha kesi zenu⛔
Kwa sababu unapokuwa umeudhika UNARUDI MWANZO MLIKOTOKA na ili uweze KUELEWA Kwanini umerudi kuwazia huko hapo ndipo utakuwa umetoka kwenye MWENDELEZO WA KUMFANYA MWENZA WAKO AWE KAMA AMBAVYO UNAOMBA AWEπ
UNAPOPENDWA USIJIAMINI SANA ETI NI HUO UZURI AMA MUONEKANO WAKO⛔
Kwa sababu MAPENZI ni maisha Basi uchukulie tu katika wajibu ki maisha,
Mbona kama ingekuwa kuna kukwepa gharama yawezekana Wewe ni gharama sana kuliko hata angenunua Mwanamke/Mwanaume ambaye yeye yupo katika mlengo huo Kwani wapo kwa gharama tofauti tofauti kuna wa laki moja na hata elfu ishilini π
Uliwahi jiuliza ni kiasi gani mwenza wako kakulinda kama MPENZI WAKEπ€·π½♂
Gharama hiyo akiamua kukudai UTAKUWA MTUMWA WAKE MPAKA UNAKUFAππ»♂
Maana yangu sio pesa ila ni UPENDO WAKE KWAKO π
Msameheane kwa maudhi yenu ila naomba niwaambie kwamba HUWEZI KUTAKA MWANAUME/MWANAMKE AWE KAMA UPENDAVYO bali ni rahisi sana kwako kumfanya Mwanaume/Mwanamke awe kama UNAVYOHITAJI AWEπ