Kuna wakati watu tunaingia kwenye MAHUSIANO/NDOA zisizokuwa na malengo ama kwa bahati mbaya au kwa kujikuta umezama penzini kulingana na MAZOEA baada ya kuwa na Mtu kwa sababu ya kampani na kumbe NDO KUJENGA MZINGA🐝
Kuachwa ni kujengwa kujipigania lakini pia ni kuelekezwa namna ambavyo UNAWEZA KUISHI PEKE YAKO.
Pengine yeye sio wa kwanza kukuacha lakini yeye ndo anaonekana kuufanya MOYO wako kuwa mpweke na wenye UPWEKE mwingi, Hakuna lililo jipya bali ni ile hali ya MAZOEA ambayo uliyajenga kwake hayo ndo yakapelekea upendo ulioutengeneza kwake huo ndo unakutesa, ni nyakati nzuri alizokupa hizo ndizo zinakuumiza kuzikosa, Lakini lazima MAISHA YAENDELEE🌍
Ukimpenda Mtu kwa hakika lazima ujue mambo makuu mawili;
▪SIKU HATAKUWEPO UTAUGUA.
▪SIKU ATAKUACHA UTAUMIA.
Kwa sababu unapompa Mtu MOYO wako maana yake anakuwa mtawala wa HISIA ZAKO na hapo ndipo matatizo huanzia, Ukimpenda mtu kwa HISIA maana yake hutapenda japo ashikwe na Mtu, Ndo Maana unakuta MAHUSIANO/NDOA nyingi watu wanasalitiana kwa sababu unaweza kuwa na MPENZI au MUME/MKE lakini hana hisia nawe, Japo anakupenda na pengine akaonyesha kukuhitaji maishani mwake but kama hana HISIA NAWE huo uhusiano/ndoa yenu ni SABABU YA MAZOEA ambayo yalitokana na namna mlivyoingia kwenye hilo penzi, mahusiano ama ndoa yenu.
Lakini akitokea ambaye ndiye wa HISIA zake ni rahisi sana wewe kusalitiwa na pengine kuachwa kabisa😭😭😭
Unajua watu wengi hawajui MADHARA ya MAZOEA lakini kwenye maisha yoyote yale hata kama unafuga PAKA🐱 ukiishamzoea Basi umejenga UPENDO kwake, Kwa tafsiri ndogo MAZOEA HUZAA KUPENDA mwisho wa yote ni wewe kuwa mhanga kwa namna yoyote ile, Ni ngumu kukwepa MAZOEA na Mtu ambaye anayazunguka maisha yako, Kikubwa NI KUWA NA KIASI hiyo inaweza kuleta nafuu pale mambo yanapokwenda ndivyo sivyo, Usimlazimishe aliyekuchoka akupe muda mwingine, Yako madhara ukilazimisha ila ukikubari KUNA UPONYAJI ikiwa utapokea kuachwa huko kama njia ya kuendelea mbele, Kuna maisha baada ya hilo ikiwa MUNGU ataweka mkono wake KUNA UWEZEKANO WA WEWE KUMPATA ALIYE SAHIHI kuliko kama ukiendelea kuumia juu ya Mtu aliyekukataa.
#Elista_Kasema_ila_Sio_She