Mwanaume mwenye gubu na masimango hufurahia sana pale ambapo anapoongea kitu na wewe kukasirika au kununa. Anapokuona unakonda kwaajili ya maneno yake au unapoenda kulalamika kwa ndugu zake kwakua tu anagubu, haachi mambo yakapita basi yeye ni kama anafika kileleni vile, raha anazozipata zinakua za ajabu hivyo hata kama akiomba msamaha vipi kua atabadilika hawezi kubadilika.
Lengo la kukununia, kukusimanga na kuwa na gubu ni ili unune na wewe kuwa na kisirani kama yeye. Kama hakupigi ni maneno tu, njia rahisi ya kupambana na kuishi kwa furaha na mwanaume kama huyu ni kumchukulia poa. Akiongea mfano, umemuambia kitu unakuta kanuna bila sababu, badala ya kuanza kuuiliza umenuna nini, mbona uko hivi, nimekuuhdi nini?
Badala ya kuingia chumbani kulia, pika chakula kizuri unachokipenda na mkaribishe mezani, kama hatakula, kula na rudi kuangalia TV. Kwa kifupi muongeleshe kama kawaida, kama hatajibu wala usijali au kuuliza kwanini amenuna, fanya mambo yako kivyako. Hata kama akinuna mwaka usimuulize kwanini umenuna, wewe si unajua ni gubu lake.
Wewe muambie kila kitu na ongea naye kama vile huoni mnuno wake. Kwanza atakua anaumia kwakua huoni mnuno wake lakini pili atajiona mjinga kununa nuna kama mtoto na ataacha, si unajua kama vile vitoto vinanuna bila sababu, ukivipuuza vinajikuta kucheka. Sasa wewe jifanye unajua kuumia na kuuliza uone kama hutachanganyikiwa.
Mtu karudi zake ofisini wala hujui kanuna nini unamuuliza hakuambii eti na wewe huli! Mtu kakosea yeye badala aombe msamaha ananuna na wewe unajikuta huna raha unanuna na kumuuliza uliza mbona huna raha mpaka inafikia hatua unaomba msamaha wewe! Dada yangu kwanini muda huo usiangalie movie, kuna matamthilia kibao au ingia hata Insta kuangalia umbea tu uone kama hatabadilika.