KWA SABABU UWEPO WAKO KWAKE UNAWEZA KUMFANYA AKAKUPENDA.
Upendo ni matendo yatokanayo na ukaribu pamoja na kujitoa, Kuna wakati Mtu unakuwa MPWEKE kwa sababu ya kukosa kile ambacho ndicho cha nafsi yako hata ukatamani kupata mtu yeyote kwa ajili ya FARAJA japo kwa urafiki wa kawaida tu, Wewe ndiye unayejua kwamba HUMHITAJI KWA UPENDO ENDELEVU bali unamhitaji kwa sababu zako mwenyewe, Ni hatari sana kwake kwa sababu yeye ATAJIKUTA AMEKUPENDA NA KUKUHITAJI UWE WAKE kutokana na ukaribu pamoja vile umejitoa kwake hivyo akija kujua malengo yako kwamba ulifanya hayo ili KUKUPA FARAJA TU utakuwa umejeruhi sana moyo wake😭😭
Lakini pia hata kwako ni HATARI kwa sababu tayari mwenzio aliishakuzoea na amejenga UPENDO kwako kwa namna yoyote inaweza kukugharimu kulingana na vile atakuwa ameumia😭😭
Vita nyingi zinazohusu MAHUSIANO/NDOA Yaani Mapenzi kwa upana wake zinatokana na UONGO
Mtu badala ya kuwa mkweli ili kuleta hoja mtu kukuelewa hata kama itakuwa ngumu kupokea huo ukweli, Wengi wanarahisisha kwa KUONGOPA ili kukwepa mijadala huku wasijue ukweli ukija kubainika ndipo itakuwa MBAYA ZAIDI
Kuliko kumkubari ama kumtaka Mtu ambaye unajua huwezi kuwa nae NI BORA KUTOKUMPA NAFASI kama ni FARAJA tafuta njia nyingine ambayo inaendana nawe ili kujipa muda wa kukabiliana na hilo ambalo linakufanya utafute FARAJA
Kwanza ni dhambi kama dhambi zingine KUDHURUMU NAFSI YA MTU hutaachwa kwenye ile HUKUMU ya USIUE Kwani wewe ni muuaji, Maana unauteka MOYO wa mtu na unaumiliki halafu Ukiona kilichokuwa kinakutesa hata kutafuta FARAJA kwake kimepata UFUMBUZI unamuacha mwenzio akiwa ANAKUPENDA wewe ni MUUAJI KAMA WAUAJI WENGINE na pengine ukawa na roho mbaya kuliko wanaotumia BUNDUKI🔫 kuua.
Kuumiza NAFSI ya Mtu asiye na hatia ni MAUAJI japo wengi hamjui, MALIPO NI HAPA HAPA DUNIANI🌍 Kikubwa UZIMA wakati wako kulipwa ukifika MWENZIO atakuwa aliishasahau na pengine amempata MJINGA mwenzie wanapeana UPENDO WA KWELI huku wewe ukipambana na malipo yako Kama ulivyotenda kwake😎
#Elista_kasema_ila_Sio_Sheria 🔨