Wengi wa walioachana na wenza wao ambao walikuwa vichomi huishia kurudiana nao na Kuanza kujutia tena na tena...
Ukiuliza sababu za kurudia maumivu majibu yao huwa mepesi sana, "Alinisumbua sana kuniomba msamaha na kuahidi kubadilika, nikamuonea huruma, ukizingatia nimeishamzoea sasa nitakuwa na wangapi!?"
Ukiuliza sababu za kurudia maumivu majibu yao huwa mepesi sana, "Alinisumbua sana kuniomba msamaha na kuahidi kubadilika, nikamuonea huruma, ukizingatia nimeishamzoea sasa nitakuwa na wangapi!?"
Mwenyewe anaiona ni sababu nzito aliyoitoa, ila anachosahau ni kuwa maumivu, manyanyaso na makwazo huwa hayafichiki kamwe, yatakuumbua ili kukukumbusha upuuzi wako wa kusamehe bila kuitazama nia yaa msamaha huo.
Sisemi kuwa usisamehe,
Ila kabla hujasamehe angalau jipe muda wa kuishi kwanza bila yeye na uone utofauti... Akiomba msamaha, muombe muda utafakari kisha uone je amebadilika kweli!?
Ila kabla hujasamehe angalau jipe muda wa kuishi kwanza bila yeye na uone utofauti... Akiomba msamaha, muombe muda utafakari kisha uone je amebadilika kweli!?
Pia kabadilika kwakuwa wewe umeondoka kwake au kwakuwa katambua kuwa anapaswa kubadilika... Kisha ndipo ufanye maamuzi sahihi na wa kujilaumu uwe mwenyewe.
Usiseme watu ni wasumbufu na ilhali wewe mwenyewe unaukaribisha huo usumbufu kwa kutokujiondoa nao!
#MkakaFulani
#MkakaFulani