-->

DADA ZANGU NI VIZURI KAMA MKIYAFAHAMU HAYA..!



Image may contain: 1 person

πŸ‘‰ Mwili wako sio Maonesho, kila
mwanaume auone.
πŸ‘‰ Mwili wako sio Mdoli kila
mwanaume Auchezee.
πŸ‘‰ Mwili wako sio dampo, upokee kila
uchafu wa mwanaume.
πŸ‘‰ Mwili wako sio Mali ya umma kila
mwanaume akutumie.
πŸ‘‰ Mwili wako sio kiburudisho, kila
mwanaume Ajiridhishe.
πŸ‘‰ Mwili wako sio pazia la Sebuleni,
kila mwanaume Akufunue.
πŸ‘‰ Mwili wako sio karanga za
kutembezwa mtaani kila mwanaume
Akuonje Utamu wako.

πŸ”Ή Mwili wako ni wa Thamani sana.
Mwili wako ndio utu wako.
πŸ”Ή Ebu Tunza Mwili wako nao
Ukutunze. Uheshimu Mwili wako nao
Utakuheshimisha.
πŸ”Ή Si kila mtu wa kuushika Mwili
wako. Usitumie Mwili wako kama
kitegauchumi, Usitumie Mwili wako
kama dhamana ya kupata vile
unavyohitaji.
πŸ”Ή Usitumie Mwili wako kama Njia ya
kupata Mume Atakayekuoa. Kama
Mungu amepanga Uolewe utaolewa tu
dada yangu hata bila ya kufunua Sketi
yako. Muamini Mungu Yeye ndiye
aliyeshikilia maisha yako.
πŸ”Ή Kuna mtu mmoja tu anayestahili
kuugusa Mwili wako, kuuona Mwili
wako, kuujua Uzuri wako.. Msubiri,
Usiwe na Haraka, Mungu atamleta
kwako. Endelea Kusubiri.

πŸ”Ή JITUNZE, JITHAMINI, JIKUBALI NA
JIAMINI..!
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU