-->

CHUKUA HII....!!


Nisikilize mimi Babe, utakapokua mjamzito, sitaruhusu ufanye jambo lolote litakalokupa stress ni mpaka utakapojifungua. Hutatakiwa kijisumbua na lolote, mimi nitakuwepo kwa ajili yako.
Please sitaki nikuone umeamka saa kumi na moja asubuhi kufanya kazi za asubuhi ikiwemo kuandaa breakfast. Hizo kazi nitafanya mimi.
Nafahamu utatakiwa kwenda clinic kila mara, nitakuwepo kukupeleka, sitakuacha uende peke yako. Daktari atakushauri kufanya mazoezi ya mara kwa mara, mimi nitakuwa 'personal Gym Instructor' wako. Nitakufanyisha mazoezi yale yanayostahili. Jioni tutatembea tembea maeneo ya karibu na tutakaporudi nitakukanda miguu yako.
Nimesikia kwamba wanawake wajawazito wanachagua sana chakula au wanapenda vyakula vya ajabu ajabu. Hata kama unataka kunywa chai iliyotiwa nazi saa tisa usiku mimi nitakuandalia.
Kila siku jioni ninaporudi kutoka kazini nitakubebea matunda uyapendayo. Unaweza usiyale ila me nitakununulia tu. Nitaku-spoil na zawadi za kutosha, na kadiri tumbo lako linavokua nitakununulia nguo zingine zinazokutosha.
Unafikiri tumeishiwa chakula? Basi usijali! Andika list ya mahitaji unayofikiri yanafaa, nitaenda sokoni kununua. Na nikiwa sokoni nitakupigia simu kukuuliza kama kuna vingine vya kununua. Sitaruhusu uende sokoni ukapigane vikumbo na watu wengi. Hauhitaji stress hata kidogo.
Umechoka kuoga? Basi nitakuogesha!
Unahisi mwili umechoka na viungo vinakuuma, nitakufanyia 'massage'.
Unataka kufungua mlango wowote ule, niite nitakufungulia!
Nitakuwa Houseboy wako mpaka pale utakapojifungua salama na mtoto akakua akiwa na afya njema.
Unaweza kuwa n wewe ndiye uliyembeba mtoto tumboni ila nitahakikisha nakusaidia kukubeba mtoto kisaikolojia kwa mapenzi na kukujali zaidi.
Wacha waseme ni Tamthiliya, mimi sijali ninachojua ni kwamba 'I love you babe' mama wa mtoto wangu wa kwanza!!!
SHARE
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU