Unapompata mtu mwenye mapenzi ya kweli, ni furaha moyoni na raha maishani!
Unaweza hisi dunia ni yako na unaweza dhani ni rahisi kuitembelea yote kwa mguu kwani haupaoni pakukushinda kwasababu dunia ya ulimwengu wa mapenzi umeshaishika.
Unaweza hisi dunia ni yako na unaweza dhani ni rahisi kuitembelea yote kwa mguu kwani haupaoni pakukushinda kwasababu dunia ya ulimwengu wa mapenzi umeshaishika.
Hata wengine walie na kusema dunia chungu kwako wewe usiku sawa na mchana. Hata bidhaa zipande bei wala hauna hofu japo kipato kidogo.
Njaa kwako inakosa heshima kwani ukilala bila kula ilimradi upo na anayekupenda basi nafsi inajilazimisha kushiba bila kula.
Watu wakilia kwasababu ya mapenzi kwako inakuwa ni ndoto kwani moyo hauna historia hiyo na kidonda kimepata dawa.
Wakisema siki hizi hakuna mapenzi ya dhati, moyo wako unasema HAPANA kwa sauti kwani upo kwenye ushuhuda wa penzi la dhati.
Wakati fulani hata una sahau madeni yote mara Mpenzi anapokuwepo nawe karibu, akiondoka unahisi mikono haina nguvu ya kufanya kazi yoyote kwani mpenzi kuondoka ni kama ameondoka na nguvu zako zote!
MUNGU AKUPE MWENZI WA KUKUPONYA MOYO, AWE FURAHA YAKO DAIMA.