-->

USIMDHARAU MTU jali UTU


Unapoona Mke wa mwanaume asiye na kazi wala kipato chochote anajifungua watoto mapacha wakati mke wa tajiri anaomba apate mtoto kwa miaka kadhaa sasa, basi Muogope sana Mungu.
.
Wakati Mhitimu wa Chuo kikuu akiajiriwa na mtu ambaye hakumaliza hata shule ya msingi basi usiidharau Elimu, bali thamini sana UTU.
.
Wakati yule mnayemuita mwanamke wa kawaida anaolewa na Mwanaume ambaye ana kila kitu katika maisha na yule mwanamke mnayemuona ni mzuri ni miaka sasa hajaolewa, basi fahamu kwamba, sio kwa uzuri au ubaya, Ndoa ni Neema tu!
.
Maisha ni safari ndefu!
.
Maisha yanafundisha Masomo yanayoumiza.
.
Fikiriria vitu unavyofanya, fikiria namna unavyowa-treat watu.
.
Kujikweza hua hakudumu. Wakati wa Malipo hufika.
.
Kile apandacho mtu ndicho atakachovuna.
.
Ubinadamu utakapeleka mbali sehemu ambapo elimu wala fedha haviwezi kukupeleka. Rehema na Baraka za Mungu zitakuinua na kufikia mahali ambapo uzuri ama majigambo hayawezi kukufikisha.
.
Kuwa mpole...haitakugarimu chochote.
.
Yusufu hakuomba kuwa waziri Mkuu wa Misri. Mariamu hakuomba kumzaa Yesu Kristo na Petro hakumualika Yesu katika boti.
.
Baraka, Rehema na huruma ziliwafuata mahala walipo.
.
Mbio za mafanikio hazijawahi kuwa ni za kibinadamu pekee ama nyota kama wengine wanavyoamini.
.
Ni Mungu pekee ndiye atakaekuchagua!
Badilika
Image may contain: 1 person, standing
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU