-->

*πŸ’—UKIWA NA MAMBO HAYA MUMEO ATAKUPENDA SANAAπŸ’—*

UTAMU KITANDANI APP
*DARASA LA MAHUSIANO*
Ni sifa 7 ambazo mwanamke‎
anatakiwa kujipamba nazo ili azidi
kumteka mwanaume, hasa mume
anayejitambua... Ni muhimu kutambua
kuwa suala la uchaguzi wa mwenza ni
jambo la kwanza kabisa kwa sababu ndio
dira ya maisha yako ya ndoa...
Je, unapaswa kuwa vipi ili mumeo
akupende?
πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—
1. MWENYE HISIA ZA UCHESHI:
Ikiwa
unafurahishwa na utani wake, ni jambo
litakalomvutia sana. Lakini ukiwa mwepesi
wa kuchukia na kukasirika, yumkini
mumeo asivutike nawe. Jitahidi kuwa na
hisia za utani na ucheshi...
πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—
2. MWENYE KUSAMEHE:
Unapoelewa kuwa
mumeo sio mtu mkamilifu na unapokuwa
na uwezo wa kumsamehe kwa dosari
zake, hii itamaanisha kuwa unamiliki
mojawapo ya sifa muhimu sana ambazo
wanaume wanazitaka kwa udi na uvumba.
Ukiwa na mchezo wa kumrukia kwa kila
kosa dogo analolifanya au ukawa na
ukosoaji uliopitiliza, tambua kuwa mumeo
hatakuwa mwenye kukufurahia, hata kama
ni miongoni mwa wale wasiosema.
Niliwahi kumnasihi memba wangu mmoja
wa Ndoa Maridhawa kuwa: “Kama
wamtafuta mume asiyekosea, hutampata
na utaishi bila mume”.
πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—
3. MWENYE SUBIRA:
Sifa hii inakaribiana na
sifa ya kusamehe niliyoielezea hapo juu.
Ninapozungumzia subira hapa
ninamaanisha uwezo wa mwanamke wa
kuwa na uhusiano na mumewe bila
kumshinikiza kuchukua maamuzi ambayo
hajajiandaa kuyachukua. Mwanamke
anaye anamuonesha mwanaume kuwa
yuko tayari kusubiri humvutia zaidi
mwanaume kuliko yule anayetoa picha
inayoonesha kuwa si mwenye subira.
πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—
4. MWENYE ASHIKI:
Mwanamke ambaye sio
romantic huwa hamvutii mwanaume. Ili
mwanaume avutike unatakiwa kumfanya
ahisi raha na uwe mwepesi wa
kumchokoza. Ikiwa unadhani kuwa
mwanaume ndiye tu anayepeswa
kukuchokoza, basi hapo unajitesa na
haitakuwa na faida kwako. Boresha uwezo
wako wa uchokozi na kuwa romantic
utaona namna mumeo atakavyokuwa
akikutamani.
πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—
5. MKWELI:
Wanaume wanavutiwa sana na
mwanamke mkweli, mwaminifu. Ikiwa
wewe ni mwanamke unayosema ukweli,
usiyeficha ukweli, basi sifa hii itamfanya
mwanaume avutike nawe. Ifanye kauli
mbiu ya maisha yako iwe ni: “Sema
unachofanya, na ufanye unachosema”.
Kama ambavyo mwanamke anampenda
sana mwanaume mkweli, vivyo hivyo
mwanaume anavutiwa na mwanamke
mkweli na mnyenyekevu ambayo hapendi
makuu.
πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—
6. ALIYEFUNGUKA KIAKILI:
Raghba ya
ugunduzi wa fikra na mawazo mapya ni
sifa nyingine ambayo mwanaume
anapenda kuiona kwa mwanamke
anayetaka kuangukia katika penzi lake.
Ninachokusudia hapa ni ule uwezo wa
kuona mbali, kutambua na kuheshimu
mtazamo mwingine, hata kama utakuwa
kinyume na mtazamo wake. Aidha,
miongoni mwa mambo ambayo wanandoa
wengi wanakosa ni dira (vision). Hakika
iwapo mwanamke ana sifa ya kuwa na
dira atamvutia sana mwanaume.
πŸ’—πŸ’—πŸ’—
7. UELEWA WA KIAFYA:
Mwanamke ambaye
anajitunza humvutia sana mwanaume
kuliko mwanamke asiyejitunza.
Muonekano wa kimwili humvutia
mwanaume. Mume huvutiwa na
mwanamke anayefanya mazoezi,
anayekula chakula chenye afya,
anayezitunza nywele zake na mwili wake
kwa ujumla, na anayevaa mavazi
maridhawa. Jitahidi sana kumvutia
mumeo kwa kuonekana mpya kila siku.

Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU