-->

Tamaa na upweke unaweza kukudanganya kuwa unampenda yule uliekutana nae.

..lakini ukweli ni kuwa kumpenda mtu ni pamoja na kumfahamu zaidi kwanza na tayari akili na moyo wako kwa pamoja vikahitaji kumpokea.
Moyo unaweza kumpokea lakini akili ikawa na maswali juu ya mtu huyo... Ruhusu moyo wako kuvumilia majibu yanayotafutwa na akili yako juu ya mtu unaehitaji kuingia nae kwenye mahusiano.. Maana usiingie kama bado akili yako ina maswali juu ya mtu huyo.
Mtu kukwambia nakupenda haitoshi kusema ndio ...bali ndio yako ije baada ya kujua mnaongea lugha moja ya upendo
Ikifika kipindi ukaingia kwenye mahusiano kwa sababu akili na moyo wako kwa pamoja vimeridhika wewe kumpenda mtu huyo, moyo wako unahisi kutaka kulinda hisia zake, akili yako inamueshimu mtu huyo.. Basi tambua wewe umekuwa kiakili na kihisia pia.
Usiruhusu tamaa na upweke wako vikakutawala maana kuna uwezekano mkubwa sana vitu hivi kukudanya kuwa unapendwa au umependa ...utakuja kujua kuwa hukuwahi kupendwa au kupenda baada ya kuingia kule ndio utajua ulikurupuka kuingia kwenye mahusiano na mtu ambae amuongei lugha moja ya upendo.. Mtu ambae ndio yako yeye anasema hapana .. Mtu ambae ndani ya muda mfupi ushaona mahusiano yenu yana matatizo mengi.
Dayari Yangu
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU