-->

#MKASA_HUU_UTAKUFUNZA_SANA_SOMA #UJIFUNZE_KITU.


Inasikitisha pole sana Irene
πŸ‘‡
Irene baada ya kufeli darasa la saba kule kijijini kwao #SONGEA alichukuliwa kufanya kazi ya HOUSEgirl jijini Dar es Salaam, alikua akilipwa elfu 40 kwa mwezi, elfu 20 alikua akiituma kwa Wazazi kijijini na 20 inayobaki anahifadhi akiba, nyumba ile alianza kukumbana na misukosuko ya kutisha ambapo Baba mwenye nyumba alikua akimlazimisha kufanya nae mapenzi wakati Mkewe na Watoto wakiwa hawapo nyumbani.
πŸ‘‡
Baba yule alimpa vitisho kuwa iwapo akitoa siri basi ndio utakua mwisho wake kukaa mjini, Irene alifikiria tabu za kijijini kwao akaamua kuvumilia, Baba yule alimpa zawadi na hela zingine za ziada kwa siri kubwa.
πŸ‘‡
Mtoto wa nyoka ni nyoka amini usiamini ila ndio hivyo, kijana wa kiume wa Baba mwenye nyumba ambaye alikuwa anasoma form 5 shule ya boys boarding akawa akirudi likizo anamlazimisha Irene kufanya mapenzi kwa vitisho vile vile kama vya Baba yake.
πŸ‘‡
Irene aliogopa sana mchezo ule mchafu anaofanya na Baba mwenye nyumba na mwanae Ali. "Hivi siku Mama Ali akijua itakuaje" alijiuliza kimoyomoyo Irene, miaka ilienda akivumilia unyanyasaji ule alipata mimba akaitoa ila bahati nzuri hakupata magonjwa, alipendeza sana Irene kwa namna familia ile ilivyomjali japo siri ya mapenzi kati yake na Baba na mwanae Ali hakuna aliyefanikiwa kuijua.
πŸ‘‡
Alitokea kijana mmoja ambaye ni dereva akajitambulisha katika familia ile na kumchumbia Irene, kwa niaba ya Wazazi wake kijijini familia ile iliridhia japo Baba mwenye nyumba alikubali kishingo upande maana ananyang'anywa tonge mdomoni, mahari ilitumwa kijijini Irene akaolewa.
πŸ‘‡
Mumewe alikua na kipato cha chini ilibidi Irene atumie hela zake alizokusanyaga kipindi cha HOUSEgirl kufungua kibanda chake cha kusajili lines pale Gongo la Mboto , siku moja alikuja kusajili line jamaa mmoja, "Naitwa Coplo Gama kusajili line ya tigo "Ni kiasi gani" Jamaa aliuliza baada ya kukaa. Irene alimjibu, "Elfu moja tu Kaka, kwani wewe ni polisi" Irene aliuliza. "Hapana mimi ni Mwanajeshi"jamaa alijibu. Wakati zoezi la usajili likiendelea, ghafla simu ya Irene iliita alipokea kumbe ni Wazazi wake waliongea kwa lugha ya KINGONI.
Irene alipomaliza kuongea na Wazazi wake Coplo Gama alimsikitikia na kumwambia, "Pole sana my kumbe mngoni mwenzangu, dunia ina shida sana ila hao ndio Wazazi wako na wanakutegemea huna budi kuwatumia chochote ulichonacho hata kama ni kidogo"
πŸ‘‡
Irene alihamaki kumbe Coplo ni mngoni na alielewa mazungumzo yote ambapo Wazazi wake kijijini walikua wakimlilia njaa na kumuomba awatumie japo chochote maana hali ni mbaya sana huko kijijini. "Kwani kwa mwezi unaingiza kiasi gani kupitia kazi hii⁉️" Coplo aliuliza. "Tigo wanatulipa laki 4 kwa mwezi" alijibu Irene."Umeolewa "Coplo aliuliza." Ndio, nina Mume na mtoto mmoja tayari "alijibu Irene." Hongera sana, una mtoto ila bado mrembo kweli kweli "Coplo alisifu." Asante"alijibu Irene.
πŸ‘‡
Maongezi yaliendelea hata baada ya zoezi la usajili wa line kukamilika, Coplo alimwambia Irene kuwa anataka amsaidie kumuingiza jeshini, Irene alifurahi kwa hoja hiyo akasema haina shida hata Mumewe atakubali tu maana ni mtu mpenda maendeleo.
πŸ‘‡
Baada ya kupeana namba za simu waliendelea kuwasiliana, ilipofika mwisho wa mwezi, Coplo alimwambia Irene aandae cheti cha kuzaliwa kopi 3, kitambulisho cha uraia kopi 2 barua ya ukazi kutoka serikali za mitaa yenye muhuri wa mjumbe na shilingi laki 3 na nusu kwa ajili ya fomu ya usaili jeshini.
πŸ‘‡
Irene alifanya yote hayo akishirikiana na Mumewe hela iliyokasoro akakopa. Coplo alimwambia Irene sasa aje nyumbani kwake siku ya Jumamosi pale Tabata ili ampe mbinu za kujibu maswali ya usaili apite moja kwa moja, Irene hakuuliza mara mbili alimuamini sana Coplo na kumchukulia kama ndugu na Kaka yake.
πŸ‘‡
Jumamosi alienda akakaribishwa ndani, baada ya story mlango ulifungwa, Coplo alimsogelea akaanza kumtomasa akamwambia, "Irene utanisamehe bure najua umeolewa ila kiukweli nakupenda sana toka siku ya kwanza nlipokuona, lazima nkusaidie uingie jeshini ila naomba japo nionje"
πŸ‘‡
Irene alibaki hajielewi alifikiri sana ila kwa kuwa ana shida na kazi alimkubalia. Baada ya mahaba mazito Coplo alimpa vijimaelekezo eti vya kujibu kwenye usaili. Irene aliondoka akiwa na huzuni ila akajipa moyo, ilikua siri yake moyoni hata Mumewe hakumwambia kuwa katafunwa.
πŸ‘‡
Baada ya wiki 3 Coplo akamwambia Irene aende tena nyumbani kwake akajaze fomu tayari ameshakuja nazo aje na passport 4 na damu kwenye kichupa kwa ajili ya vipimo ila akamsihi hatomfanyia chochote kama siku ile ya kwanza. Irene alienda akijipa moyo kuwa sasa zoezi linaelekea mwisho hivyo huzuni ile ya mwanzo itaisha, alipewa fomu za kujaza kweli ila baada ya zoezi Coplo akamfosi tena wafanye mapenzi kwa mara ya mwisho Irene hakuwa na cha kujizuia, alipigwa mtama chali kitandani akashughulikiwa.
πŸ‘‡
Irene aliondoka, baada ya mwezi Coplo alimuita, wakiwa sebuleni Coplo akijifanya analia na kusikitika alimwambia Irene, "Vipimo vya damu yako vimeonyesha uliwahi kutoa mimba kwa hiyo ombi lako la kuingia jeshini limekataliwa" Irene alihamaki, Coplo alimtimua, akiwa na huzuni zaidi,Irene njiani alilia sana akimlilia Mungu, "Kwa nini mimi eeh Mola⁉️" alifika nyumbani ila Mumewe siku ile aligundua Mkewe hayupo sawa, alimbana akamwambia, "Niambie kila kitu nini umefanywa huko na huyo Coplo‼️‼️⁉️ na kama huniambii nakupa talaka leo leo".
πŸ‘‡
Kwa uchungu huku akilia Irene aliamua kukiri yaliyotokea Mumewe alisikitika mno ila akamwambia, "YOTE HAYA NI SABABU YA SHIDA ZETU MKE WANGU, ILA MUNGU YUPO ATATULIPIA".
πŸ‘‡
Baada ya miezi kadhaa Irene alidhoofu kwa mawazo akifikiria muda na fedha alizopoteza kwa ajili ya utapeli wa Coplo. Irene aliugua alipopelekwa hospitali alipimwa na kukutwa amepata maambukizi ya virusi vya ukimwi, Mumewe pia alipima akakutwa nae ameshaambukizwa ukimwi, ilikua ni kilio kikubwa sana ila Mumewe alimfariji akamwambia, "USIJALI MKE WANGU, NAJUA UNAJUTIA KULETA MAUTI KATIKA NDOA YETU ILA NAJUA HUKUPENDA, ULIDANGANYIKA KUTOKANA NA UMASIKINI WETU, NAAHIDI SITOKUACHA NTAKUFA NAWE, USILIE TULIA TUMLEE MTOTO WETU HADI HAPO KIFO KITAPOTUFIKA".
πŸ‘‡
Irene alilia sana na kumuomba msamaha Mumewe, baada ya wiki 2 Irene alichanganyikiwa akawa taahira anazurura mitaani akilia, Mumewe alianza kutumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi ARV na hadi muda huu anaendelea kumlea mtoto vizuri alozaa na Mkewe Irene.
πŸ‘‡
Skendo ile ilivuma wasamaria wema wakapeleka taarifa polisi Coplo akakamatwa akakiri akafukuzwa kazi kwa aibu baada ya mwezi mmoja akajinyonga akaacha ujumbe usemao, "NAFSI IMENISUTA, NMEDHULUMU NAFSI ZISIZO NA HATIA, BORA NIFE".
#Funzo
Kama wewe ni MWANAUME jiulize ni nafsi za WANAWAKE wangapi unazidhulumu au umezizulumuJiulize wewe ni kama Baba mwenye nyumba au , mwanae Ali au Coplo Gama
Tambua malipo ni hapa hapa duniani na MWENYENZI MUNGU πŸ‘‡ anakuona kwa dhuluma unazowafanyia WANAWAKE na MABINTI wa watu ipo siku utajutia.
Binti jiulize unatumia njia zipi kutatua shida zako⁉️ Je Unafanya kama Irene au
Ni vema binti kuepuka kutumia mwili wako kimapenzi kama njia ya kutatua matatizo yako yasijekukukuta matatizo makubwa zaidi hata ya hayo uliyofikiri unayatatua.
Kama umeguswa kwa namna moja au nyingine na mkasa huu na ungependa uwafikie watu wengi zaidi katika jamii tafadhali πŸ™ SHARE STRAIGHT AWAY WITHOUT DELAYS
πŸ‘πŸΎπŸ‘€πŸ‘‚#NZINGATIOπŸ‘‡
❤️ NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE NA MALAZI YAWE SAFI MAANA WAASHERATI NA WAZINZI MUNGU ATAWAHUKUMIA ADHABU
(WAEBRANIA 13: 4)
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU