-->

Kutembea na mume wa mtu sio jambo zuri japo wanawake wengi wanaona ni kawaida bila kujua wanajilimbikizia laana itakayofanya maisha yao kuwa magumu mbeleni.


Machozi ya uchungu ya mwanamke mwenzio juu ya mume wake hayafutiki haraka. Ni kama zigo la kinyesi mgongoni linavutiwa na inzi pekeake.
Huyo mwanaume unaemuona leo ana mke, pesa na mali na kuona ndio fursa kwako kumpata kwasababu anajua kujali na anapesa za kutosha kukugharamia. Ukirudi nyuma miaka 10-15-20 mwanaume huyo huyo alikuwa kama huyu wako unae mkataa leo.Unaye muona hajui kuvaa, hana pesa za kutosha, hana mali kwahiyo hakufai.
Wanaume wengi wanaanzia chini... Jitihada za wake zao zinawafikisha hapo walipo leo. Heshimu jitihada hizo. Heshimu siku walizofunga kwa ajili ya waume zao, heshimu machozi waliomlilia Mungu awafikishe walipo, heshimu muda na jasho walilolitoa kuhakikisha waume zao wanaonekana watu mbele za watu.
Muombe Mungu akupe wa kwako hata kama masikini mpate utajiri pamoja. Na wewe upige magoti, ulie na kufunga.
Wanawake wengi wanalalamika hawaolewi au wachumba wanawaacha bila sababu za msingi. Wanasahau zigo la kinyesi walilobeba mgongoni mwao. Mwanamke piga magoti muombe Mungu akusamehe kwa kumliza mwanamke mwenzio.
Tuwaombee watoto wetu na kuwaonyesha njia iliyo bora. Kuwafundisha dini ili wawe na mahusiano mazuri na Mungu wasikumbwe na laana hii.
Ewe mama elimisha watoto wako. Ewe dada elimisha wadogo zako. Mume wa mtu si mali yako tafuta wakwako.
ITUNZE NDOA YAKO whatsApp Group 0717 442 212.
Au bonyeza link hapo chini ikupeleke moja kwa moja kwenye whatsApp inbox yangu
👇👇👇
https://wa.me/255717442212
Share
Like Page
Image may contain: 1 person, standing and outdoor
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU