-->

Acha kujiumiza moyo wako kwa kujaribu kulazimisha mahusiano ambayo kimsingi hayawezi kuendelea.

Hauwezi ukamlazimisha mtu kukupenda hata siku moja, hauwezi ukamlazimisha mtu akujali! Huwezi ukamlazimisha mtu awe muaminifu katika mahusiano yenu kama kufanya usaliti ni hulka yake huwezi ibadili. Hauwezi ukamfanya mtu awe vile unavyotaka wewe awe.
Muda mwingine mtu unaemuhitaji sana ni yule ambaye ni bora zaidi kama hutokuwa nae. Inabidi ujaribu kuelewa tu kwamba mambo mengine yamepangwa yatokee. Mambo mengine huja katika maisha yako lakini si kwa madhumuni ya kukaa na kudumu. Usijihangaishe kwa kujaribu kufix kile ambacho kilipangwa kivunjike tu.
Hauwezi kupata uhusiano wenye afya kwa mtu unaemuhitaji ambaye yeye binafsi hawezi kufanya hivyo. Iko hivi, kama ukiwa mvumilivu ku move on na maisha yako utakuja kuelewa kwanini ilikuwa hivyo, na huenda ukajiona ulikua mpumbavu kupoteza muda kwa mtu asie kujali hata chembe.
NIAMINI MIMI! Usiwekeze furaha yako kwa mtu ambae kimsingi hawezi kuitunza furaha yako. Kurasa nyingine hutakiwa kufungwa na maisha lazima yaendelee.
Ungana nasi katika group letu la whatsApp "ITUNZE NDOA YAKO" ili upate njia bora za kutunza na kuimarisha Ndoa, Uchumba/Mahusizno yako kwa kunitumia ujumbe wako kwenye whatsApp inbox yangu kwa nambari 0717 442 212.
Au bonyeza link hapo chini ikupeleke moja kwa moja kwenye whatsApp inbox yangu
👇👇👇
Share
Like Page
Image may contain: 2 people, people standing
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU