-->

Kama ujui majukumu ya ndoa usijaribu kuingia ili ufurahishe ndugu,jamaa na marafiki.


Usiingie kufuata mkumbo wa fulani,rafiki yako ameoa au ameolewa.
Usijaribu kuigusa ndoa kama uyajui majukumu yako ndani ya ndoa.
Kwa sababu,chanzo cha mahusiano mengi ndani ya ndoa yanavurugwa na baadhi ya watu wanaingia kwenye sekta pana na ni agizo la mwenyezi Mungu kwa kukimbilia tu na hawana utashi wa kuidumisha ndoa.
sio jambo la umri wa mtu,wala si jambo la kufundishwa,kupenda au kumchukia mtu sio elimu inafundishwa mashuleni,kama ndivyo hivyo basi wote wanaofundwa au makungwi ndoa zao zingedumu mpaka kifo.
ni jambo linatoka kwenye moyo wa mtu.
kujitambua,kujikosoa mwenyewe,hapa nipo sahihi au nimekosea na kujisawazisha.
kama mtoto kichanga afundishwagi kula,kumpenda mtu sio jambo la kufundisha eti leo nataka mwanangu umpende binti JANGALA,
Kuna mtu au watu,wapo kwenye ndoa lakini kulitamka neno nakupenda,ahsante,nisamehe,mume wake au mke wangu ni ngumu.
Lugha ya mahaba hana,lugha ya faraghani hana,kama jeshini ukali mpaka kwenye faragha.
Jamani simba mwenyewe mkali lakini ikifika muda wa faragha anasalendar,mpole kama ananyolewa.
Jambazi pamoja na ukatili wake ikifika kwenye masuala ya mapendeko anatulia,mpole hatari.
ANGALIZO
Jambo la ndoa halibaki kwa tukio moja,mawili tu eti kusex na kuzaa,hapana.
Ndoa ni sekta kubwa,kuna vikolombwezo lukuki na vyote tunapaswa kuvitekeleza.
Jukumu la baba liwe la baba kusiwepo kukwepa au kutega.
Na jukumu la mama libaki kuwa la mama asikwepe majukumu.
Narudia tena na tena,kama ujui misingi,majukumu ya ndoa usiingie,mnachafua hali ya hewa.
Image may contain: 2 people
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU