Kwa wale wenye kusikia wito na moto ndani yao ya kuanzisha maono na huduma kwaajili ya kumtumikia Mungu zingatia haya;
1:Usianzishe huduma ili kwamba uje kupata hela kupitia huduma maana utaachia huduma njiani,Nadal take katika Maono wewe ndiye unatakiwa uwe mtoaji mkubwa na wala sio mpokeaji.
2:Usianzishe huduma kwa kutafuta kuja kuheshimiwa na watu maana wakati mwingine itakuwa vise versa,unaweza usipate heshima stahiki hasa kama watu hawajakulewa na kujua nguvu iliyopo ndani yako.Matokeo yake utataka kuitafuta heshima kwa nguvu na kwa garama.
3:Usianzishe huduma ili watu wakutumikie,huduma ni kuwatumikia watu sio wao wakutumikie.
4:Usianzishe huduma kwa nia ya kutaka kusikia kusifiwa na kupongezwa.Mara nyingine na wakati mwingine utajikuta unapokea lawama,shutuma na kutokusifiwa.
ZAIDI
Usije kujaribu kujiita kwenye huduma mwenyewe kama hujaitwa na Mungu,ukiija kwenye huduma uwe na uhakika utaishia njiani,neema ya kumaliza hutakuwa nayo.
Huduma sio lele mama,kama hunielewi kamsome Musa katika safari yake ya huduma ya kuwaongoza Israeli
Kasome waliyopitia Mitume na manabii,je uko tayari?
Kasome waliyopitia Mitume na manabii,je uko tayari?
Naweza kukutia Moyo wewe uliyeitwa na Mungu kweli kweli Mungu atakupa heshima,baba atakusifu na atakupa stahiki yako.Unaweza usivipate vitu hivi kwa wale unaowangoza lakini Mungu ni mwaminifu na waki ukapanda mema utavuna tu mema hata kama sio kwa pale ulipopanda. Na mwisho wa yote utavikwa taji ya uzima.
Winnie Nzobakenga Kilemo