-->

KABLA YA KUINGIA KWENYE NDOA TAFADHALI ZINGATIA HILI

Kabla hujaelekea katika Ndoa, usijisahau ukataka kulazimisha Mtu akupende wakati kimsingi hana hisia na wewe.
.
Mtu sahihi anayekupenda, atakuonesha tu kwa vitendo. Maneno ni rahisi mno kuyatamka. Usiamini kila neno litokalo mdomoni, tizama matendo zaidi.
.
Mtu anayekupenda na mwenye ndoto njema na wewe utamuona tu na wala moyo wako hautajaa mashaka ya kujiuliza uelekeo wako.
.
Kama ni wewe pekee unayelazimisha kiasi umakini, kwamba unalazimisha kupiga simu, unalazimisha kujibiwa text, unalazimisha kuonana, hiyo iwe dalili kubwa ya kukuonesha huo uelekeo hauna tija yoyote kwenye maisha yako zaidi ya maumivu.
.
Kama anakupa sababu kibao za kukaa mbali na wewe, iwe jibu kwako kwamba hana ndoto njema zozote na wewe.
.
Mtu anayekupenda umakini huja bila kulazimisha kutoka kwake. Usiwe kipofu ukaongozwa na kipofu mwenzio, maana, itakuwa rahisi mno kuingizwa shimoni na humo ndipo utakapoharibu maisha yako.
MWANDISHI ðŸ‘Œ Dr Naomi Andrew
.
Image may contain: 1 person, selfie and close-up, text that says "Usilazimishe Mapenzi"
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU