1. KUBALI KOSA: Usiendelee kumzungusha Wife wakati unajua umemkosea ๐คซ๐คซ.
2. OMBA MSAMAHA: Omba msamaha kwa kumaanisha hadi Wife ajue unajutia kosa ๐๐ฝ๐๐ฝ.
3. USIRUDIE KOSA LILELILE: Kurudia kosa moja kila wakati inamaanisha hakuna toba ya kweli ๐๐.
4. USIJARIBU KUJITETEA KWA KUMKUMBUSHA WIFE MAKOSA YAKE: Hata kama Wife alishawahi kukukosea na ukamsamehe; usilete hiyo mada hapo Brother! Wewe kuwa MPOLE tu ndugu yangu, shughulikia AGENDA iliyopo mezani ๐ค๐ค.
5. KIPINDI CHA TOBA MFANYIE WIFE VITU ANAPENDAGA: Wewe unajua anachopenda Wife wako; fanya kwa bidii kama sehemu ya toba. Mfano kumpikia (kama unajua lakini), outing, kusafisha nyumba, kumsaidia watoto, nk!! Mara nyingine ni ngumu kufanya haya mambo ila jitahidi iwe ENDELEVU ๐ท๐ท.
6. MWAMBIE WIFE AKUOMBEE: Yani akikubali KUKUOMBEA baassiiii; umesamehewa kabisaaa ๐๐. Unajua mtu hawezi kukuombea kwa MUNGU pasipo kukusamehe kwanza ๐๐.
โจNB:
๐ UKIKAA VIBAYA NA WIFE KILA KITU KINAGOMA!
๐ Happy WIFE... Happy LIFE!!
1 PETRO 3:7; โKadhalika ninyi WANAUME, kaeni na WAKE ZENU kwa AKILI; na kumpa mke HESHIMA, kama chombo kisicho na nguvu; maana wao pia ni warithi wa neema ya uzima, ili MAOMBI yenu YASIZUILIWE na chochote.โ