-->

UKIONDOKA KAMA MTUMWA RUDI KAMA SHUJAA



MADE IN TANZANIA!!! – Nuru The Light
Ukiondoka sehemu kama mtumwa hakikisha unarudi kama Shujaa, kwa sababu ukiondoka na ukarudi kama ulivyokuwa mwanzo watazidisha mbili mara mbili itazaa nne.
Kama dharau ilikuwa asilimia mbili itakuwa asilimia nne.
Wakikuambia ondoka hapa hatukutaki waambie asante huenda wamekuepusha na mengi.
Unadhani Yusufu angekuwa Waziri Mkuu Misri akama asingeuzwa kama mtumwa?
Lakini hao hao waliomuuza walikuja wakamsujudia kama Kiongozi wao na yeye ndo akawa msemaji wa mwisho wa masuala ya kifamilia na Taifa la Misri. Kutoka utumwa hadi ufalme.
Kuna rafiki yangu alinihadithia kisa cha jamaa mmoja aliyekuwa akipata kila kitu toka kwa Kaka yake hapo mwanzo baada ya wazazi wake kufariki.
Ilifika kipindi bila kukosana yaani Kaka yake akajisikia tu kumfukuza kwake.
Jamaa akajua Kaka yake anatania kumbe alikuwa serious.
Akamtupia mabegi nje, huku Shemeji mtu naye akiwa haamini kama shemeji anafukuzwa nyumbani bila kosa lolote.
Kaka yake alikuwa na fedha za kutosha hivyo kuwa na gari ya kupigia misele kwa jamaa ilikuwa kawaida tu.
Anasema aliishi maisha ya taabu sana baada ya kutimuliwa na kila alipompigia Kaka yake simu hakupokea na mara atumiapo simu nyingine na kujitambulisha Kaka humkatia simu.
Akaja kupata dili la kuchukuliwa na tajiri mmoja wa Madini ya Tanzanite kule Mirerani. Akafanya kazi kule lakini baadae aliamua kuingia mwenyewe binafsi akapambane na baadae alikuja kufanikiwa kupata jiwe la maana.
Akauza yale madini na kuanzisha biashara zake huku ikiwa imepita miaka 12 bila kuonana na Kaka yake kwa sababu alivyoona Kaka hana msaada wowote kwake akaamua kupoteza mawasiliano naye.
Alifungua biashara kubwa sana na za maana, akaamua kurudi kwa Kaka yake akapiga magoti na kumshukuru.
Kaka yake akamjibu kuwa mdogo wangu sisi hatuna wazazi, tumebaki mimi na wewe, nilikuwa najitahidi nakupa kiasi fulani cha pesa lakini ukawa haujiongezi nikaona haukui, hivyo uamuzi sahihi ulikuwa ni kukutimua ukaone maisha ya kitaa yalivyo na upambane mwenyewe maana sikutaka nije nigeuke mlishaji wa familia yako.
Hivyo hata Yusufu kama angeendelea kuishi pale na kudekezwa na Baba yake Mzee Yakobo hata siku moja asingekuja kuwa Waziri Mkuu.
Nikajifunza kumbe kuna mambo yanakuja ya kuudhi na kukatisha tamaa lakini katika hayo Mungu amekusudia tuweze kuwa watu wenye uvumilivu, ustahimilivu, saburi na wenye utu.
Ili dhahabu ing’ae nasikia kuwa lazima ipitishwe kwenye moto.
Mungu akiamua kukuheshimisha acha kabisa.
Walikutimua wakiwa wanakulipa laki tatu baadae wanakuomba radhi na urudi kazini kwa mshahara wa milioni Mbili
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU