-->

KILA NINAPOINGIA KULALA NINAPOANZA KUFIKIRIA KUHUSU MAHISHA NINAGUNDUA KWAMBA :-




BONYEZA HAPA KUPAKUA APP YA UTAMU KITANDANI UJIFUNZE MENGI KUHUSU MAPENZI 
Kila ninapoingia kulala ninapoanza kufikiria kuhusu maisha.Nina gundua kuwa:
Muda fulani ili ufanikiwe unahitaji maadui....utashangaa lakini ni NDIO unahitaji.
Unahitaji watu wakukuumiza ili ukumbuke kukimbilia kwa Mungu.
Unahitaji watu wa kukuudhi ili uwe na hasira.
Unahitaji watu wa kukuambia HAPANA ili ujifunze kujitegemea.....namaanisha ufanye mwenyewe.
Unahitaji watu wa kukusaliti ili tumaini lako uweke kwa Mungu.
Unahitaji watu wa kukuchongea upoteze kazi yako ili ugundue kipawa ulichonacho na uanzishe biashara yako kubwa.
Unahitaji watu wa kukuuza kama Yusufu kule Misri ili ukawe waziri katika nchi ya kigeni.
Unahitaji mwenye nyumba mjeuri,ili usiwe na amani katika nyumba ya kupanga ili ujitahidi kujenga nyumba yako haraka.
Lakini muda mwingine tunapokatishwa tamaa,tunajihisi vibaya,tunabaki katika hali hiyo.Hatujui kuwa mwisho wa kukatishwa tamaa ndio mwanzo wa mafanikio yako.
Tambua hili "kila ukatishwaji tamaa uliokutana nao ulikuja na baraka!" Ijapokuwa siyo kila mmoja ataona katika maana ninayoieleza.
Huwezi kuona mlango MPYA uliofunguka kama bado unakazia akili,muda na nguvu kupambana kufungua ule uliofunga.
Narudia tena kukukumbusha "Hakuna ukatishwaji tamaa usiokuja na baraka.
Kwa hiyo unapojikuta katika hali hiyo endelea kufurahi,tumia akili,ifungue macho uone mpango mpya uliowazi.
Kukatatamaa ni HATUA moja,kufanikiwa ni hatua ya pili,nina mashaka ikiwa kuna yeyote anayeweza kuruka hatua ya kwanza.
Ndiyo sababu inaitwa KUKATA-TAMAA ni lazima kwanza UKATE ndipo uende katika kutimiza TAMAA.
ANZA SASA!


BONYEZA HAPA KUPAKUA APP YA UTAMU KITANDANI UJIFUNZE MENGI KUHUSU MAPENZI 
Malipo ya dharau na manyanyaso.
Kupata nafasi ya kuishi ni upendeleo tosha.
Kabla haujachukua hatua za kumnyanyasa mtu au kumdharau fikiria kuwa u mavumbi na kuna wakati utakufa na kusahaulika katika uso wa dunia.
Kabla haujamnyanyasa yatima kumbuka kuwa duniani tunapita na maisha ni mzunguko huenda huyo unayemnyanyasa ndio atakuwa mlezi wako uzeeni.
Kabla haujamnyanyasa mjane na kumpokonya Mali kumbuka kuwa huenda wanae siku moja wakaja kuajiri wanao.
Kabla haujamtelekeza mwanao na kwenda kuoa/ kuolewa fikiria na jifunze kwa mifano juu ya wale waliotelekezwa na wakafanikiwa kimaisha. Nafikiri unajua nini huwa kinatokea.
Usimkatae mwanaume/mke kwa mwonekano wa nje au hali yake ya kiuchumi ya sasa, huenda siku moja akaja kuwa mwajiri wa mwenzi wako, yeye ndo akawa mtu anayefanya muone mipango yenu inaenda.
Angalia ana nini anacho fikiri kwa maisha ya baadae na sio ana nini mkononi.
Alishawahi kuongea Mandela kuwa "utakapomkataa mwanaume/mke mwenye maono na ukaamua kuolewa/kuoa na mwenye luninga ndani (Mali) ipo siku utakuja kumwona mwenye maono(mipango) kupitia luninga ya mumeo/mkeo.
Uzee raha ukizeeka na amani na sio kuufanya ndio muda wa kujuta na kutubu.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU