Tendo la ndoa ni kitu ambacho watu hudhani kuwa kinatakiwa kufanywa usiku. Naam, unaweza kufanya tendo la ndoa muda wowote, lakini ukweli ni kwamba kulifanya tendo la ndoa usiku tu inaweza kutengeneza uchoshi kwa wanandoa.
*FAIDA ZA TENDO LA NDOA LA ASUBUHI*
Bila shaka utafurahi ukijua kwamba tendo la ndoa la asubuhi (kiamshio) sio tu kwamba ni jambo zuri, bali pia litakusaidia kimwili, kiakili na kiroho. Famasia yako ya Ndoa inakuletea baadhi ya sababu za umuhimu wa kufanya tendo hilo asubuhi mara kwa mara:
*1. URAHISI NA WEPESI:*
Wengi wetu tunapenda kulala kwa kujinafasi, huku tukiwa na nguo kidogo mwilini. Wengine hulala bila nguo kabisa, na nilieleza faida zake katika somo la FAIDA ZA KULALA BILA NGUO. Tendo la ndoa la asubuhi hukufanya usihitaji kuvua nguo, jambo ambalo kwa nyakati nyingine itakulazimu kuvua mzigo wa nguo.
Aidha, tendo la ndoa la asubuhi huwafanya mnapoingia bafuni kujisikia raha na ladha ya kipekee.
*2. UBORA:*
Tendo la ndoa la asubuhi ni bora kuliko wakati mwingine kwa sababu kadhaa. Mosi, nishati, utuvu na utulivu wa kiasili huwafanya kuwa na stamina kubwa ya kufanya vizuri na kuwafikisha kileleni kwa raha ya aina yake. Wanandoa wanaofanya tendo usiku kwa kawaida huwa wamechoka kutokana na shughuli za kutwa nzima, na hivyo kufanya viungo vyao kuwa na mwitikio mdogo wa kimahabba.
Pili, dakika chache baada ya kuamka, akili yako inakuwa bado haijaamka, na hivyo inakuwa haijakutana na mambo mengi. Matokeo yake, jambo hilo linaweza kukufanya kuwa kama bepari wa mahabba kitandani.
*3. WAKATI WA DHAHABU:*
Nuru maridhawa ya asubuhi huongeza nuru na mng’aro wenu huku mvuto ukiwatamalaki na kuongeza umaridadi wenu. Hakika hamu ya tendo katika wakati huo wa dhahabu huwafanya mhisi ukaribu usiomithilika.
*4. MKURUNGE WA ASUBUHI:*
Bila shaka utakuwa umeshuhudia wanaume wengi wakisimamisha wakati wa asubuhi. Mumeo huamka akiwa amesimamisha mkurunge wake kwa sababu ya mzunguko wa asili wa homoni ya kiume ya testosterone. Ubongo wa mwanaume huusambazia mwili kiwango kikubwa cha testosterone kila asubuhi, hivyo kuufanya mkurunge wake usimame na kuonesha uhai.
Hiyo ina maana kuwa uwezo wake pia unakuwa mkubwa na anaweza kufanya vizuri zaidi huku msisimko wa tendo ukiwa mkubwa sana na kuifanya asubuhi yake kuanza vizuri.
*5. SIKU NZIMA UTAJISIKIA VIZURI:*
Tendo la ndoa huufanya ubongo wa mwanadamu kutoa maada za serotonin na dopamine, ambazo kazi yake kubwa ni kumpa mtu hisia za utuvu na utulivu. Aidha, anapofika kileleni ubongo hutoa maada iitwayo, ambayo kazi yake hukufanya uhisi kuwa na ukaribu mwanana na mpenzi wako. Hili ni jambo muhimu sana ambalo litaing’arisha siku yako na kuifanya kuwa maridhawa.
*6. HUONGEZA UMARIDADI WAKO:*
Licha ya raha ya tendo inayotokana na kufika kileleni, tendo la ndoa huweza kukupa faida kayaya za kimwili ikiwa ni pamoja na mng’aro, nuru na umaridadi. Maada zitokanazo na tendo huzifanya nywele zako kung’ara, ngozi yako kuchanua na wajihi na macho yako kuwa na utuvu na utulivu. Tunaweza kusema kuwa tendo la ndoa la asubuhi ni dawa nzuri ya urembo kuliko gharama kubwa za vipodozi na urembo wa saluni.
Nawatakia utekelezaji mwema.
*7. HUONGEZA UTENDAJI WA UBONGO:*
*7. HUONGEZA UTENDAJI WA UBONGO:*
Tendo la ndoa la asubuhi hukupa siku yenye tija kazini, kwa maana shughuli ile ya kitandani huuamsha moja kwa moja ubongo kwa kuchochea utendaji kazi wa mwili wako. Mzunguko na utendaji kazi wa mwili wako huufanya ubongo wako upokee kiwango kikubwa cha oxygen na virutubisho vinavyotakiwa na vya kuupa nguvu ya kufanya kazi barabara. Matokeo yake, utakuwa makini zaidi, utakuwa na nishati zaidi, na utakuwa na ubunifu zaidi.
*8. NI ZOEZI ZURI:*
Tendo la ndoa la asubuhi ni mbadala mzuri wa kwenda gym au jogging ya mtaani. Tendo la ndoa hupunguza kiwango cha kalori sawa na kile kinchopunguzwa na jog kwa dakika 30. Uzuri zaidi ni kwamba unakuwa pamoja na kipenzi chako, hivyo unapata kufurahia upendo huku ukichoma kalori bila kunyanyuka na kwenda nje.
*9. HUONGEZA HAMU YA KULA (appetite):*
Bila shaka kifungua kinywa ndio mlo muhimu kabisa wa siku yako. Tendo la ndoa la asubuhi ni zoezi na huongeza hamu, jambo litakalokufanya uwe na hamu ya chakula. Aidha, homoni za endorphins zinazotolewa wakati wa tendo hukupa uhakika wa ladha nzuri ya chakula.
*10. HUCHANGAMSHA NDOA NA MAHABBA YENU:*
Tendo la ndoa la asubuhi huongeza chachu na msisimko kwenye uhusiano wa ndoa yako kwa njia nyingi. Kwanza, kujua kwamba unaweza kufanya tendo la ndoa mwanzo wa siku bila kipingamizi huonesha kwamba kuna mahabba motomoto bado yanarindima kati yenu.
Pili, kuianza siku yako kwa kitu kitamu cha kimahabba humfanya kila mmoja wenu amuwaze mwenzake kwa siku nzima.
Tatu, itakufanya kufanya mabadiliko ya mazoea yako ambapo badala ya kukimbilia kwenye masufuria ya vitumbua na maandazi, unaanza na kiamshio mwanana cha kimahabba.
*Nakutakieni utekelezaji mwema.*