-->

MWANAUME MWENZANGU LITAMBUE HILIπŸ‘‡:


Image may contain: 1 person, sitting
🌺 Mke ni Sawa Kabisa na Mwili Wako (Hata Binadamu Wa Kwanza/Adam Alikiri hili ninalokueleza (Soma Mwanzo 2:23) Utajionea)

Adam Alipozinduka Tu Toka Usingizini Alisema "Huyu ni MFUPA wa MIFUPA Yangu Na NYAMA Ya NYAMA Zangu, Hapohapo Akampa na Jina Kwamba Ataitwa MWANAMKE Kwa Maana Alitokana na Mwanaume"

🌺 Pia Elewa Kwamba Mwanamke ni Msaidizi Wako...Yani Kwa Maana Nyingine Mwanamke ni KIKAMILISHO Chako Wewe Mwanaume.

HIVYOπŸ‘‡:

🌺 Umpigapo Mwanamke Tambua unajipiga Wewe Mwenyewe.😁😁

🌺 Umnyanyasapo Mwanamke Tambua Pia Ni Sawa na Unajinyanyasa Wewe MwenyeweπŸ˜€

🌺 Hata Ukimsimanga Mwanamke Wewe Tambua Tu Unajisimanga Wewe MwenyeweπŸ˜…πŸ˜…

🌺 Yani Ukimfanyia UOVU Wowote Mwanamke Wewe Tambua tu ni Sawa na Unajiumiza Wewe mwenyewe...Maana Mwanamke Ni MFUPA Katika MIFUPA yako na NYAMA Katika NYAMA Zako.

CHA KUKUSHAURI MWANAUME MWENZANGUπŸ‘‡:

🌺Hivi Viumbe Inabidi Tuendelee Tu Kuishi Navyo Kwa Akili Kama Mtume Paulo Alivyotusihi kufanya Hivyo (1Petro 3:7)

NA KUISHI NAVYO KWA AKILI KULIKOMAANISHWA NDIKO HUKUπŸ‘‡:

🌺 Kwanza Wapeni Heshima Wake zenu Kama Chombo Dhahifu Sana yani kwa maana nyingine Mwanamke ili tu Dua/sala zenu zipate kufika Kwa Mungu.

🌺 Pili, Msilipe Ubaya Kwa Ubaya Juu Yao Wake Zenu

🌺 Tatu, Muwe na Huruma na Unyenyekevu Wa Hali ya Juu Sana Kwa Wake Zenu.

🌺 Nne, Muwe na Hisia na Upendo Wa Kindugu na Wake Zenu.

🌺 Tano, Tusipende Ku-Mind kila Vitu Vidogo Vidogo Kwa Wake Zetu Vingine Tuache Vipite.

ZINGATI: WANAWAKE WANAOLENGWA HAPO πŸ‘† NI WAKE ZETU WA NDOA HALALI KABISA NA SIYO MICHEPUKO, πŸ˜πŸ˜MICHEPUKO MWENDO NI ULEULE WA KUSURUBISHWA TU πŸ˜πŸ˜HUKU MKINGOJEA HUKUMU YENU SIKU YA MWISHO,
πŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒ
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU