Wiki iliyopita nilikua nasafari, kuna rafiki zangu wawili nilikua nasafari nao, kwenye saa 11 na nusu za asubuhi niliwapitia wote, kila mmoja kivyake, tukaondoka na nilimuacha kila mmoja alipokua anaelekea. Kila mmoja alikua na safari yake na mmoja alikua akienda kwa mume wake ambaye anaishi mikoa tofauti, nilifika nikakutana na mume wake tukasalimiana, wakati wakurudi kama siku tatu baadaye nilimpitia na mume wake ndiyo alimleta nikarudi nao wote.
Tulirudi usiku, hivyo nilimpeleka mmoja mmoja mpaka nyumbani. Wakati tunarudi nikawa nawaambia kuwa usimfuatilie mpenzi wako ambaye hamuishi pamoja kwakua ukichunguza sana utaambiwa kuwa anachepuka. Alibisha, akaniambia mapenzi bila kumchunga mpenzi wako basi utaibia. Nilimuuliza, mimi na wewe sio wapenzi, lakini nimekuja kukuchukua nyumbani kwako sa akumi na moja na nusu asubuhi.
Kama kwa mfano ulikua hujamuambia mume wako au mume wako alikua hanijui, jirano yako akaona, angesema huyu kaja kuchukuliwa na mwanaume saa kumi na moja asubuhi, nimekurudisha baada ya weekend tena usiku, hivi mtu kama huyo akisema “Kuna jamaa ambaye anakuja kumchukua kila jumamosi, wanaondoka anamrudisha jumatatu tena usiku. Akaelezewa vizuri huyo mtu si ataamini kuwa tunachepuka? Aliniambia ndio, mume wako kweli kama asingekua ananijua angeamini ni rafiki?
Jibu lilikua ni hapana? Lakini huyo jirani aliyeona kwani kasema uongo? Maana ni kweli nilikuchukua asubuhi, nikakurudisha baada ya siku tatu, usiku tena weekend? Hajui tumeenda wapi lakini si atawaza tu kuwa kuna kitu? Jibu lilikua ni ndiyo hata mimi nitawaza kuna kitu! Vipi siku nyiongine akikuona mjini upo kwenye gari yangu, tumekaa sehemu tunakula, tumekutana tunasalimiana, si ndiyo atasema kuwa hata mapenzi yetu hayajifichi kila siku tuko pamoja, akasema ndioyo.
Nikamuambia basi ndiyo hivyo, ukimfuatilia sana mpenzi wako lazima atakua anachepuka hata kama hachepuki. Watu wanaokuambia niliona mwanaume/mwanamke akiingia chumbani kwa mpenzi wako hawajui walikua wanafanya nini? Hawajui huyo ni nani? Mhukumu mpenzi wako kwa kile anachokuonyesha na si kwa maneno ya watu. Kama hajawahi kukuonyesha kama anachepuka kwanini kulazimishia kisa jirani kakuambia? Jirania anaelewa kile anachokiona na si uhalisia, mhukumu kwa matendo anayokuonyesha wewe na si kwa maneno unayosikia!