-->

JE NI KWELI KUMEZA DAWA YA FRAGIL BAADA YA TENDO LA NDOA INAZUIA KUPATA MIMBA?


Fragil inafanyaje kazi?
Dawa hii ni ya kuua vijidudu vilivyo kwenye group la gram negative.. dawa hii inafanya kazi kwa kuharibu au kuvuruga mpangilio wa vinasaba vya wadudu hawa (DNA) na kuwaua.
Inapoingia mwilini haibadiriki inabakia kuwa hvyo hivyo Metronidazole na inasambaa sehemu zote za mwili ikiwemo damu,mate,kizazi, placenta(kwa wajawazito) na ubongo.
Baada ya masaa 7 inaanza kupingua mwilini kwani Ini linaitoa kupitia mkojo ndani ya masaa 24 inakua imeisha. Na inapokua kwenye mkojo inatoka vile vile haibadiliki kuwa kitu kingine.
*JE INAWEZA KUZUIA MIMBA?*
ili kuzuia mimba inahitaji kubadili hali ya ute uwe mzito kuruhusu mbegu kufikia yai na kuongeza hali ya asidi ya ute wa ukeni na kwenye kizazi. Mbegu za kiume zinaweza kustahimili PH kuanzia 2.5 kuendelea ute unapokua na PH ndogo zaidi ya hapo basi mbegu hizi zikiingia zinakufa. Ndo hvo dawa za uzazi wa mpango za dharura na dawa za kuua mbegu zinavofanya kazi.
Baada ya kuangalia hayo tuone Fragili (metronidazole) ina PH ya ngapi? Kama nlivosema inapoingia mwilini inasambaa kama ilivyo haibadiliki kuwa kemikali nyingine Na Dawa hii inapoyeyuka kwenye maji inakua na PH ya 6.5 hvyo hata ikiingia kwenye ute haishushi PH kuathiri mazingira rafiki ya mbegu. Na pia haiathiri ute wa uke kuzuia mbegu kuweza kuogelea.
Hivyo basi dawa hii haizuii mimba.
Bali inakuweka kwenye hatari ya kuzaa mtoto mwenye mapungufu endapo mimba itatunga kipindi umemeza dawa hii.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU