-->

AMANI YA MOYO NI MUHIMU KULIKO PENZI LA MSALITI* MUACHE AENDE!

Impande zitatu z'urukundo abakundana bahana - TUYAGE URUKUNDO
• Kamwe usihisi kama ulimwengu ndio unakaribia mwisho pale akupendae anapokuacha.
*MUACHE AENDE*

• Kujaribu kumlazimisha mtu akupende ni sawa na kujaribu kumlazimisha bata wachafu kutambua usafi na uzuri. Usimlazimishe akupende, mwache mwenyewe akupende, kama hakupendi...
*MWACHE AENDE !*

• Wewe ni wa thamani mno kulilia penzi. Mtu ambae anakupenda kweli atakuheshimu na hataku 'treat' kama uchafu. Kama atakuchukulia wewe kama uchafu...
*MUACHE AENDE !*

• Usipoteze muda wako wa thamani kujaribu kumshawishi au kuomba mapenzi. Mtu mwingine pembeni anakupenda wewe kwa dhati, ila wewe uko busy mno kumuogesha bata maji Kwanini?
*MUACHE AENDE !*

• Usikasirike pale mtu wako anapompenda mwingine tofauti na wewe. Siku zote hua ni vigumu kumshawishi ```NYANI``` kwamba Asali ni tamu kuliko ndizi...hata kaka Mwalimu Bemasha Bemastasha Shauri na page zake zinazoongoza kwa makala nzuri Facebook na Youtube kwa sasa Tanzania anasistiza kila siku.
*MUACHE AENDE !*

• Mwanamke/mwanaume yeyote anaekuchukulia kirahisi siku zote atachukulia faida kwako, atakugeuza atakavyo kama chapati akijua hufurukuti, yeye sio Mungu wa kukufanya atakavyo...
*MUACHE AENDE !*

• Kuna watu hawatakupenda hata kama utajitoa kiasi gani kwao. Ni sawa tu. Kukukataa kwao haimaanishi kwamba una kitu kibaya, bali ni maana kwamba hawako kwa ajili yako. Usilazimishe duara kuwa pembe tatu...
Na unaamini hukumkosea basi usiumie sana mungu yupo na ni niwakwetu sote lazima tu alipe kwa aliyofanya hata kama ni lini..
*MUACHE AENDE !*

_CHA KUJIFUNZA_
• Hauwezi badilisha maoni mabaya ya watu juu yako, ila unaweza ukazuia maoni yao mabaya yasikubadilishe wewe kama wewe!
• Acha kichwa chako kiongoze moyo wako kukuondoa katika mahusiano sumu. Lengo la mahusiano sio kuleta mafadhaiko ila ni kuongeza furaha juu ya ile uliyokuwa nayo mwanzoni ulipokuwa haupo katika mahusiano.

NI NGUMU SANA ILA KWA MUSTAKABALI WA FURAHA YAKO YA SASA NA YA BAADAE MIMI NAKWAMBIA *MUACHE AENDE* MPE KINYWAJI NA NAULI KABISA!
Kama ipo ipo tuuu...!

tuache muda uamue wenyewe🙌🏿
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU