-->

Uzuri wako unamkabidhi nan? Unajua kwamba ukikosea kuwa na mtu sahihi kwenye mahusiano unaweza ukashindwa hata kuona thamani ya uzuri wako?

Uzuri wako unamkabidhi nan? Unajua kwamba ukikosea kuwa na mtu sahihi kwenye mahusiano unaweza ukashindwa hata kuona thamani ya uzuri wako?
Tukiachana na uzuri wa nje tambua kwamba una uzuri wa ndani ambao utakufanya uthaminike na pia kuheshimiwa na yeyote. Mwanamke unatakiwa kuwa kama sumaku! Sumaku inavuta vitu vya chuma tu hivyo nawe yakubidi umvutie mwanaume mwenye sifa na vigezo vya kujali utu na sio vitu.
Mwanaume mwenye hofu ya Mungu, busara, anayetenda matendo mema na mwenye upendo, kujali na moyo safi.
Mwanamke ukitaka uzuri wako ununuliwe na vitu, mwonekano pamoja na umaarufu usije kulalamika utakapoumizwa na kupotezewa muda.
Kumuomba Mungu akupe mwanaume sahihi ni jambo jema sana ila usiishie tu hapo bali tumia na akili aliyokupa Mungu kumjua huyo aliye sahihi kwako. Fedha na mali za wanaume kisiwe kigezo cha kumpa usahihi mwanaume.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU