-->

SABABU SITA ZA WANAUME KUTOKUWA WAAMINIFU/ KUCHEPUKA KWENYE MAHUSIANO

SABABU SITA ZA WANAUME KUCHEPUKA

MAPENZI – Page 61 – My Blog

1. Utaalamu wa masuala ya mahusiano waonyesha dhairi kuwa Mwanaume huanzisha mahusiano ya nje anapoona Mke wake hamsifii na anamkosoa kila mara. Wanaume waliohojiwa wanasema: πŸ‘‡πŸ‘‡

“Nilianza kuhisi Mke wangu ameanza kuniona sivutii tena, alikuwa ananikosoa, mara viatu vinanuka, mara sijachomekea shati,”

Hivyo wanasema wanahitaji kutendewa kama Wafalme, wasifiwe, waambiwe ni ‘bomba’ kwenye tendo la ndoa.

2. Kumdhani anachepuka wakati hafanyi hivyo. Hilo humfanya Mume achepuke tu hata kama hakupenda.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Tony (siyo jina lake halisi) anasema, “Mke wangu alianza kuhisi nachepuka wakati wa fungate, kila mara alinihisi hivyo na wakati sikuwa na mahusiano yoyote,” baadaye nikaamua kuchepuka kweli.

3. Anatafuta rafiki. Wanaume wengi wanapokosa Mke ambaye watacheka, watapiga stories, watataniana, wanapendelea movie za aina moja, wanazungumzia mambo yao, huamua kwenda nje kutafuta Watu wa aina hiyo. πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Wapo Wanawake ambao kila Mume anaporudi humpokea na maswali, kumsakama alikuwa wapi, kumuorodheshea mahitaji ya nyumba. Wanaume wanadai wanapenda faraja.

4. Wanataka mzuka. Mtaalamu wa mahusiano Mely Morse, anasema katika siku za kwanza za mahusiano, kila mmoja huwa na hamu na mwenzake, lakini kadri muda unavyokwenda mnazoeana.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Wanaume wana tabia ya kutafuta mzuka wa tendo kwa kitu kipya. Hiyo ni hulka yao.

5. Morse anasema wanaume wengine huchepuka kwa sababu tu ni wadhaifu.
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Wanapokutana na mitego ya Wanawake wazuri, kama baa, kazini au club, wanashindwa kukataa au kuzuia hisia zao.

6. Penda usipende, Wanaume wengine wanachepuka kwa sababu wanataka ladha tofauti.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Si kwamba hampendi Mke wake, la hasha wanataka kuona Mwanamke mwingine atakuwaje.

Ndio maana Wokovu ni Dawa ya Moyo , bila Wokovu moyoni Mwanadamu hawezi kushinda vishawishi vya shetani bila YESU πŸ™ kuishi moyoni mwake , maana yupo Roho Mtakatifu msaidizi wetu sote , ndiye atusaidie kulijua Neno la MUNGU πŸ™ vema , na kuishi katika Neno la MUNGU

πŸ”΄NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE πŸ™
NA MALAZI YAWE SAFI πŸ™
Umejifunza kitu?
SHARE na Wengine
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU