π️Ukweli ni kwamba NDOA haikimbiwi, ukiingia umeingia, NDOA ni kama mfano maji uliyoyavulia nguo kwa maana utayaooga tu ikiwa tayari upo kwenye Ndoa ni kuendelea tu. Pale unapoona watu ambao ni Wazee kwenye NDOA ujue kuna mengi wamepitia ndio maana hata sasa bado wakidunda.
π️Ukifanikiwa kuongea na Mwanandoa mkongwe atakueleza siri zilizowafanya kufikia umri huo wa Ndoa.
π️ Lakini Ndoa si Ndoa bali Ndoa yenye kujengwa kwenye msingi imara wa Mungu hiyo ndio NDOA ninayoizungumzia hapa.
π️ Hivyo ni vyema ujifunze siri hizi za kuinogesha NDOA yako / kuiomarisha NDOA yako ( to build a great marriage).
✍️Siri zipo nyingi, lakini siri zote zimefungwa kwenye neno moja, nalo ni;
❤️Upendo.
“Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria.Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako.Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.” Warumi 13:8-10
“Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria.Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako.Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.” Warumi 13:8-10
✍️Neno linaeleza kwamba, usisumbuliwe na mambo mengine yoyote isipokuwa kupenda tu. Kwenye NDOA ni vivyo hivyo, usisumbukie kutengeneza sheria ili Ndoa yako iwe sawa, bali wewe PENDA tu/ PENDO lako la dhati li juu ya sheria zote. Kwa sababu ukipenda hutakubali kumuumiza mpenzi Mume/Mke wako, hutakubali kumsononesha Mpenzi Mume/Mke wako, hutakubali kumpiga, hutakubali kumfanyia hila nakadhalika. Ukweli ni kwamba ;Ukimpenda Mumeo ujue umeitimiza sheria na Mumeo ni vivyo hivyo. Kwa maana hutaitajika kuambiwa “usinzini, usiue, usitamani, na amri nyingine yoyote” bali ukipenda moja kwa moja huwezi kumwibia mwenzako penzi lake na kushea na mtu mwingine, tena huwezi kutamani nakadhalika.
✍️Kumbuka Pendo halimfanyii jirani ( mpenzi wako Mume/Mke) neno baya, kwa kuwa pendo ndilo utimilifu wa sheria.
✍️Umeshawahi kuona mtu anampenda mwandani wake kuliko ajipendavyo mwenyewe❓ Ndio wapo watu wa namna hii. Je unafikiri mtu wa namna hii, kweli ataweza kumsononesha, kumpiga au kumtenda mambo ya hiyana mwandani wake❓ Jibu ni hapana, hawezi kuthubutu kumfanyia ujinga mwenzake.
✍️ Kumbe shida ya ndoa yako ni kukosekana kwa pendo halisi, na huo ndio ukweli.
✍️Matokeo ya kukosekana kwa pendo la kweli ndani ya NDOA ndio tunayaona magomvi yasiyoisha, chuki, adhabu ya kunyimana unyumba, kelele na matukano yasiyoisha, mauaji nakadhalika
✍️Biblia inasema “… Pendo ndilo utimilifu wa sheria “ikiwa na maana hakuna sheria yoyote itakayosimama kwa mwenye pendo. Huwezi kumwambia Mkeo / Mumeo “ kuwa Mwaminifu ” bali akipenda / akiwa ndani ya pendo ni lazima atakuwa mwaminifu kwako.
✍️ Ssasa umegundua shida iliyopo❓ Ni moja tu, “PENDO halipo kwenye ndoa” na PENDO sio tendo la ndoa, au kumshikashika Mumeo hadi waambiwa usimshike atakuwa "malinda "huo sio UKWELI kwa mtazamo wangu π naona si vema kuwafundisha Wanawake Mawazo hayo potofu , useme kwamba “ kwa sababu ninampa Mume wangu kila wakati akihitaji, hivyo nampenda , sio sex yenye kupima UPENDO ❤️” ( na Mume ni vivyo hivyo sio mabao ya nguvu unayomfunga Mkeo ndio UPENDO ❤️). PENDO ni zaidi ya tendo la ndoa❗ Ingawa “ PENDO ” ndio mworobaini / dawa yenyewe ya kuboresha NDOA yako, lakini ni vyema nikuchambulie moja moja ambalo litaboresha au kujenga ndoa yako kuwa ndoa babu kubwa! Nayo ni ;
Mweshimu MUME/MKE
✍️Naliwaona Wanandoa fulani ambao kwa kweli hawaeshimiani hata kidogo.
✍️Na kwa sababu hiyo Ndoa ilikuwa chungu badala ya kuwa tamu.
✍️ Mume alimdharau Mkewe na Mke naye akamdharau Mumewe. Ilikuwa ni hivi;ππ π Mwanaume anamwita Mkewe maneno ya ajabu ajabu, Mwanaume anawakumbuka Wanawake zake wa zamani aliokuwa nao, akifikiri kwamba walikuwa wakimweshimu sasa bahati mbaya amejisahau kwamba Yeye sasa ni Mume wa mtu na ameokoka.
✍️ Mke wake baada ya kuona dharau zimezidi, naye “ akamtupa kapuni” ( hakumjali kwa lolote) Jamani, waswahili wanasema ;
✍️“ Heshima ni kitu cha bure, haiuzwi! ” jifunze kumheshimu mwandani wako katika mambo yote.
✍️ Jukumu la “ heshima ndani ya Ndoa ” sio suala la mtu mmoja tu. Bali kila mmoja na ajifunze kumweshimu mwenzake. Mara nyingi katika utamaduni wetu wa kiafrika tunakosea, kwa maana tumekuwa na mtazamo mbaya juu ya neno “heshima” tukidhani kuwa heshima ni kutii. Na tunafikiri Mke ni lazima amweshimu Mumewe na hatujui kwamba na Mume anapaswa amweshimu Mkewe. Heshima sio utii, bali ni hali ya kumtanguliza mtu kuwa anafaa zaidi.
Hakikisha UNAWAACHA WAZAZI / WALEZI.
✍️Siku moja, Wanandoa fulani walikuwa na mpango wa kununua shamba eneo fulani hivi, wakawa na mpango wa kujenga pia.
✍️Mipango hii ilikuwa ni ya Wanandoa hao. Lakini Mwanaume alikuwa na desturi ya kumuuliza Mama yake katika yote waliyopanga na Mkewe.
✍️Sasa akamwuuliza “ Mama mimi na mwenzangu tunataka kununua shamba na maeneo hayo hayo tujenge huko “ Mama yake alikataa hayo maamuzi yao “ hapana sitaki mwende kujenga huko, wala hamna sababu ya kujenga kwa sasa, nitawaambia muda sahihi wa kujenga… “
✍️Bπasi yule kijana, akatoka hapo na maamuzi ya Mama yake. Alipofika kwa Mke wake, akapangua mipango yao.
✍️πππ Sasa hali hii iliwasumbua sana hata kupelekea magomvi ndani ya Ndoa yao. Je unafikiri huyu Mwanaume amewaacha Wazazi wake kweli❓
✍️ Hapana bado yupo na Wazazi wake kwenye Ndoa❗
✍️ Ni kweli Wazazi wanasehemu yao muhimu sana kwenye Ndoa, wao wameyaona mengi hata wakati mwingine wakikushauri yafaa kabisa kufanya hivyo.
✍️Lakini isiwe kwamba mamlaka ya kimaamuzi yatoke kwao, hapo ndipo kuna makosa.π
✍️Wazazi wakiwa ndio wasemaji wa mwisho katika mipango yenu, ujue ilo ni tatizo baya sana. Ili uweze kuijenga imara Ndoa yako yakupasa uwaache Wazazi, na uhakikishe maamuzi, mipango, mambo yenu yanabakia ya kwenu kwenu isipokuwa pale tu inapobidi kuomba msaada zaidi kwa Wazazi iwe hivyo.
✍️ Baba na Mama yako na wenyewe wanayakwao, na isikute yakwao yenyewe yanawashinda❗
✍️Wao ni Wazazi na sehemu yao ipo pale pale, lakini isizidi ya hapo.
✍️ Hujawahi kuona mtu akigombana na Mpenzi ❤️ Mume π/Mkeπ wake kwa sababu Mzazi ameingia sana kwa mambo ya Watoto❓
✍️ Ndio zipo ndoa zinazopitia majanga kwa sababu mmoja hajaamua kuwaacha Wazazi wake.
✍️ Ebu jihoji jambo hili kwenye Ndoa yako limekaaje❓ Je wewe upo sawa❓ Au Mpenzi ❤️ Mume/Mke wako je amefaulu kuwaacha Wazazi / Walezi au jamaa zake wakaribu❓
✍️Wakati mwingine sio Wazazi tu, hata ndugu au jamaa zako wa karibu kama Marafiki, hao wote hawapaswi kuwa wenye sauti kwenye Ndoa yenu.
✍️ Hujawahi ona jinsi ambavyo marafiki wanavyochangia kuharibu ndoa❓
✍️ Ni kweli marafiki wanaweza kuchangia vizuri kuijenga Ndoa yako, lakini sehemu kubwa ya mchango wa marafiki ni kubomoa na sio kuijenga Ndoa.
✍️Sasa angalia kile utakachopanga au kujadili na Mpenzi ❤️ Mume/Mke wako, alafu pembeni awepo rafiki ambaye wewe humjui lakini kinyemela yupo pamoja na Mpenzi ❤️ Mume/Mke wako huko wanapokutana.
✍️Angalia tabia ya Mpenzi ❤️ Mume/Mke wako itakavyokuwa, angalia mipango yenu itakavyokuwa, alafu uniambie kama mambo hajaenda kombo❗
✍️Ifike wakati sasa, uachane wale wa nje ambao wamekuwa na nafasi ya kushauri mambo ya Ndoa yako na wakitaka ufanye hivyo.
✍️ Ndoa ni ya kwako na mpenzi / Mwanandoa wako. Usipoweza kuwaacha Wazazi kwenye fikra zako, ujue Ndoa π haitaweza kuimarika.
✍️Fanya maamuzi leo kwamba maamuzi yenu yaendeshwe na ninyi wenyewe…π
NDOA π NA IHESHIMIWE NA watu WOTE NA MALAZI YAWE SAFI π MAANA waasherati na wazinzi MUNGU ATAWAHUKUMIA adhabu (Waebrania 13:4)