-->

MWANAMKE NA MWANAUME WANA WAJIBU WENYE KUHESHIMIKA💓💓


Ukiona njigi utadhani njege na ukiona njege utadhani njigi!😃 Uchunguzi nilioufanya katika mitandao ya kijamii nimegundua kuna chuki kali kwa wanaume dhidi ya wanawake. Malalamiko ni mengi mno. Mwanamke analaaniwa analaumiwa amepewa kila aina ya sifa mbaya kana kwamba mwanamke ndio chanzo cha matatizo yote yanayotokea ulimwrnguni. Jambo hili lilianza tangu mwanzoni mwa historia ya mwanadamu. Wakati Adamu alipoulizwa kwa nini alikula tunda alilokatazwa badala ya kukiiri kosa na kuomba msamaha Adamu alimlaumu mke wake "mwanamke ulienipa alinishawishi nami nikala" likuwa ni kama vile Adamu anamlaumu Mungu kwa kumpa mke! Ni km alikuwa akisema " bila wewe kunipa huyu mwanamke nisingeasi😃😃😃😃 je Mungu alisikiliza utetezi wa Adamu? Hapana! Wote wawili Adamu na mke wake walifukuzwa katika bustani ya edeni na wote walipoteza ukamilifu wakawa wanaumwa kuzeeka na kufa. Adamu alimsikiliza mkewe kuliko Mungu. Wengi wanahisi aliogopa mkewe atamnyima😊😊upumbavu
Tangu wakati huo wanaume wamekuwa ni watu wa kuwalaumu wanawake tena kwa udhaifu wao wenyewe. Yaani ni watu wa ajabu mno. Wanalalamika ooh hakuna wanawake mabikira siku hizi! Sasa wanaume mabikira wapo? Hizo bikira wanawake walitolewa na nani? Yaani wewe umeshatumika afu unataka kitu kipya? Hakuna mwanamke bikira bila mwanaume bikira HAKUNA! Ummpate wapi? Huna haki hata ya kuwaza yaani upumbavu kwa sababu hakuna palipoandikwa kuwa mwanaume afanye ngono kabla ya ndoa bali wote walipewa sheria moja tu na wote wanapaswa kubaki safi mpk ndoa. Hivyo kutarajia uoe bikira huku wewe ushatumika ni ndoto za mwendawazimu. HUWEZI kujaza divai mpya kwenye viriba vikuukuu.
Afu utawasikia eti wanawake ni malaya mapenzi wanataka pesa! Lakini hivi kuna mwanaume utamwambia ngono isubiri ndoa akubali! Thubutu! Na uking'ang'ania msimamo wako mapenzi yanaisha! Anataka ngono haramu tena bure. Tangu lini vitu haramu vikapatikana bure? Kwa hiyo huna haja ya kumuoa unataka starehe tu nae atataka hela hakuna starehe isiyo na gharama! Unauza dhahabu feki unalipwa noti feki ngoma droo! Wanawake wanajiuza. Nani anawanunua km sio nyie wanaume? Hakuna biashara bila mnunuzi! Hivyo km Adamu wanaume mlipaswa kuwa na msimamo dunia haingekuwa hivi hasa ukizingatia Mungu alimpa mamlaka mwanaume dhidi ya mwanamke. Mwanaume ni kiongozi alitakiwa awe mfano wa kuiga. Hata mlaumu na kulaani bado mwanamke hamuwezi kumkwepa. Mwanaume ni km teja kwa mwanamke. Heshimuni uumbaji
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU