-->

Jinsi Ya Kunyoa Ndevu kwa Ufanisi na Kuepukana na Vipele ..!!!

Jinsi Ya Kunyoa Ndevu kwa Ufanisi na Kuepukana na Vipele ...

Moja ya matatizo makubwa kwa wanaume ni unyoaji wa ndevu, kitu ambacho wakati mwingine huwakera wahusika na wao kujiona kama ni wafungwa. Ndevu huwafanya wanaume wengi kuhisi kuwa ni tatizo kubwa sana kwao kwani wakati wa kuzinyoa huwa ni tatizo kubwa kutokana na wengine kuweza kupata matatizo wakati wa kunyoa ndevu.
Ili kuondoa matatizo haya yafuatayo yanaweza kabisa kukusaidia kukuweka katika aina Fulani ya raha kubwa. Chagua mashine ya kunyolea na wembe ambao unadhani unaswihi ngozi yako, kuna aina nyingi sana za mashine za kunyolea pamoja na nyembe zake ni muhimu kujua wembe ambao unatumia kwa kuzingatia mahitaji yako hasa ya aina ya ndevu.
Weka uso safi na usio mchafu, Safisha kabla ya kunyoa, hii inakusaidia kufungua matundu yanayoshikilia ndevu kabla ya kunyoa ili kuweza kupata mnyoo laini na wenye uhakika.
Usisahau kuloweka kidevu chako vyema, hii inasaidia wenye kupita kiulaini zaidi na kama unatumia kiwembe cha kawaida basi ni vyema sana kufanya kazi hiyo ukitoka kuoga.
Tumia maji ya moto siyo yanayounguza kama inawezekana, yanasaidia sana kufungua vishimo vya vinyweleo, pia unaweza kupata masaji ya chapchap katika uso ili kusaidia kulainisha kidevu chako.
Chagua krimu hasa inayostahili kwako ya kunyolea kwa kutegemea ngozi yako na chagua linalostahili unalotaka, jipake kiasi cha kutosha katika sehemu zinazostahili kwani husaidia kuburudisha ngozi.
Baada ya kujinyoa, osha uso wako na ondoa krimu zote,tumia moistrurizer baada ya kunyoa.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU