-->

ZINDUKA ACHA KUKUBALI KUISHI NA MTU AU KUMZALIA ZALIA MTU AMBAYE HUMJUI!

Image result for mapenzi wakubwa
Mwanaume ana miaka zaidi ya 30, hajaoa lakini ameanza kufanya kazi miaka mingi, labda ana miaka mitano kazini, ndiyo wewe umemuona na amehamia sehemu ulipo, hujui chochote kuhusu yeye zaidi ya ule uongo anaokuambia. Mmekaa kwenye mahusiano mwezi mmoja anakuambia anataka muishi pamoja au anakuambia anataka umzalie!
Dada yangu kwakua na wewe una kizazi chako na aunatamani ndoa sana unakubali. Hufikirii hata mara mbili, hata hujiongezi kua huyu mtu ambaye yuko na haraka ya kusihi pamoja hata miezi mitatu bado, sijui chochote kuhusu yeye, ndioyo kaja hapa tena sio katoka chuoni katoka kazini. Hujiulizi je huko alikotoka alikua haishi na mwanamke?
Hujiulizi kwanini hataki kuoa anazungumzia kuishi pamoja na kuzaa kirahisi rahisi hivi kama vile ni kwenda kununua vocha na kujiunga na kifuruishi. Huwazi hivi mtu ambaye anaonekana kabisa ni kicheche maana mimi mwenyewe kanitongoza na kunipata kirahisi kweli alikua single? Lakini hujiulizi hivi kama alikua na mtu inamaana hao wanawake wengine hawakutaka kuishi naye au hawakua na vizazi?
Wakati mwingine unaweza kuona umeokota Dodo chini ya Mkukumanga lakini dada yangu utakuja kulia tu! Sisemi umkatae lakini hembu chunguza kidogo, angalia basi hata ujue kwao, si kwakukutambulisha hapana lakini kabla ya kuishi na mtu ujue hata kwao wapi, ujue hata ndugu au rafiki mmoja ambaye anamjua tangu zamani. Kama basi nawewe una hamu hivyo ya ndoa basi hembu fanya hivi, ingia basi hata kwenye ukurasa wake wa Facebook au Instagram na angalia Post zake.
Nina uhakika kuna mtoto kapostiwa au kuna angalau dada mmoja alimuambia Happy Birthday Love na kasahau kuifuta. Narudia kuwa makini, huko alikotoka kulikua na wasichana tena ogopa zaidi kama akikuambia kuna mwanamke nilizaa naye lakini hatuko pamoja. Hapo mara nyingi ni kama anakuambia “Nina mwanamke mwingine nilikua naishi naye hivyo sitaki usumbufu pale utakapoona meseji zake au simu za kutaka matumizi.” Sana sana atakuambia ni X wangu anasumbua hataki tuachane.
Kama sauti haitoshi ni mseme tu!
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU