-->

HUNA MAISHA BINAFSI UNABOA LAZIMA UTAISHIA KUACHWA!

Image result for mapenzi wakubwa
Hakuna wanawake wanaboa na ambao ni wagumu kuwa nao kwenye mahusiano kama wanawake ambao hawana maisha yao binafsi. Hapa nazungumzia mwanamke ambaye hana marafiki wenzake wakike ambao atapiga nao umbea au dada zake wakugombana nao anataka akipata Boyfriend mbali na kua mpenzi wake, awe shoga yake na dada yake, hana maisha yake binafsi hivyo anadhani na wewe huna maisha yako unamuwaza wewe.
Amekupigia simu mara tatu kwa siku lakini bado analalamika humtafuti, anataka kila mkitoka uwe naye, kila akikuona online anataka uchat nayeye. Unasikia wanalalamika “Nimekuona online lakini hujibu SMS zangu. Yaani mna miezi mitatu lakini anataka kila kitu unachofanya umuambie, yaani anataka muda wote uwe kuhusu yeye. Huyu ni mwanamke ambaye alikua mpweke, alikua hana rafiki hivyo akipata mwanaume anataka amgande awe dada yake, awe pia na rafiki yake.
Kama una tabia hizi basi kuachika ni mwezi mmoja tu, kama huwezi kupitisha siku nzima bila kumpigia simu na akikupigia usilalamike basi jua wewe unaboa. Kama mwanamke ni lazima uwe na kitu kingine cha kukupa furaha, hapa nikimaanisha kuwa, uwe na furaha ndiyo utafute mwanaume na si kutafuta mwanaume wa kukupa furaha. Kwamba uwe na uwezo wa kutoka out mwenyewe na si kukaa ndani ukisubiri mwanaume wa kukutoa out.
Unapokua mpweke, unapokua huna kitu kingine cha kukupa furaha basi jua utataka mwanaume kuchat na wewe kila wakati, uatataka asiwe na marafiki, utataka awe anakushirikisha mipango yake yote ya maendeleo, awe anakuja kwako au uwe unaenda kwake kila siku. Kama ndiyo mnaanza mahusiano ushakua hivyo basi hata mimi sitakuweza, ni mwezi tu nakuambia Mama nina maisha yangu katafute yako kwanza ndiyo uje, hakuna mtu anataka kazi ya kukufariji na kutaka kukufurahisha kila saa.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU