-->

WEWE NI KISIRANI KAMA KILA SIKU UNAKUMBUSHIA MAKOSA YA ZAMANI;

 Image result for mapenzi wakubwa

Mtu anayelalamika ni mtu ambaye hasahau kitu kinapotokea, mume au mke anapofanya makosa badala ya kumhukumu kutokana na makosa ya wakati huo basi hukumbushia makosa ya zamani na kumhukumu nayo, kwake hakuna kitu kinapita. Kwa mfano mwenza wako kachelewa kurudi nyumbani, kwa mtu ambaye anaongea atasema hivi;
“Mbona leo umechelewa, nilijaribu kukupigia simu yako haipatikani? Vipi huko kazini…ulikua wapi mpaka saa hizi?” Huyu ataongea, atasubiria jibu, hata kama mhusika ni kawaida yake kuchelewa lakini hatakumbushia kuchelewa kwake kwa jana. Lakini mtu anayelalamika atasema “Nimechoka na tabia yako, mambo gani haya kila siku kunijia usiku, juzi ulikuja hivi, tangu tuoane hujawahi, tangu sijui lini unakuja usiku!”
Hahukumu kuchelewa kwa siku ile, akasikiliza labda kweli mtu ni mchelewaji, lakini siku husika inawezekana hata alikua na tatizo la kweli, labda anaumwa, labda kulikua na mgonjwa, labda kasimamishwa kazi na mambo kama hayo. Wewe unabeba kuchelewa kwa miaka kumi iliyopita unakulete siku hiyo. Sasa kwakua mtu hatachelewa siku moja tu basi anasema kuwa kazi yako ni kulalamika.
Kama unaongea na mtu na unataka akusikilize kweli nilazima ujifunze kuacha kabisa kukumbushia makosa ya zamani hasa kama mhusika ulishamsamehe. Unapokumbushia makosa ya zamani haisaidii, inamfanya mhusika kukuzoea na badala ya kujiona mkosaji akaomba msamaha basi hukuona kama una kisirani kwani unakumbushia vitu ambavyo yeye ashavisahau na hawezi kuomba msamaha kila siku kwa kosa lilelile.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU